Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi wakati akizungumza na Menejimenti na watumishi wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania katika Makao Makuu ya taasisi hiyo jijini Dar es Salaam tar 20/7/2026 ambapo lego kubwa lilikuwa ni kukutana na kuweka mikakati ya utekelezaji wa mambo mbalimbali kwa mwaka huu mpya wa fedha ambapo amesisitiza Makumbusho ya Taifa kuimarisha mchango wake kwa Taifa
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga akizungumza na Menejimenti na watumishi wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania katika Makao Makuu ya taasisi hiyo jijini Dar es Salaam leo tar 20/7/2026
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika onesho la kudumu la ndege ya kwanza ya Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere tar 20/7/2026
Picha ya pamoja kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga pamoja na watendaji wa Makumbusho ya Taifa pamoja an wadau mbalimbali.
Dkt. Abbasi, ambaye amepokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Dkt. Noel Biseko Lwoga, amesema Makumbusho ya Taifa ni taasisi muhimu yenye jukumu la kuhifadhi historia, utamaduni na urithi wa Taifa, huku akisisitiza kuwa mchango wa sekta hiyo unapaswa kuonekana katika maendeleo ya nchi.
“Sekta hii ina mchango wake kwa jamii, siasa na uchumi, na mchango huo unatakiwa uonekane. Misingi imara inatakiwa kuwekwa ili taasisi iweze kutimiza wajibu wake kwa ufanisi,” amesema Dkt. Abbasi.
Amesema ni muhimu kuimarisha misingi ya taasisi kwa kuweka mikakati endelevu ya kuongeza mapato na kushirikisha wadau katika shughuli za kuhifadhi na kuendeleza urithi wa Taifa.
Aidha, amekielekeza Kitengo cha Masoko na Uhusiano kuandaa programu mbalimbali za masoko na utangazaji zitakazoongeza mwonekano wa Makumbusho ya Taifa, kuvutia wageni wengi zaidi na kuongeza mapato ya taasisi.
Dkt. Abbasi amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Makumbusho ya Taifa kwa kutoa ushirikiano na msaada unaohitajika ili kuboresha huduma, kuimarisha uhifadhi wa urithi wa Taifa na kuongeza mchango wa taasisi hiyo katika maendeleo ya uchumi wa nchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga ametumia fursa hiyo kusema kuwa Makumbusho itaendelea kufanya tafiti,kuihifadhi na kuielimisha jamii kuhusu urithi wa utamaduni.
Baada ya kikao hicho, Katibu Mkuu ametembelea onesho la kudumu la ndege ya kwanza ya Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambapo alielekeza kufanyika maboresho zaidi ya eneo hilo ili wageni wapate fursa bora ya kujifunza historia ya chombo hicho cha kipekee na nafasi yake katika historia ya Taifa hasa tunapoelekea katika mashindano ya AFCON 2027.
SOMA MAKALA NYINGINE MUHIMU HAPA
Magazeti ya leo Jumanne 21 Julai 2026,
Rais Samia ashiriki Kikao cha Baraza la Uongozi la Umoja wa Afrika.
Wafungwa 1,036 Wasamehewa Kwa Msamaha wa Rais Samia
Waziri Ridhiwani Kikwete aipongeza (TEA)kwa huduma Bora kwa wananchi
Waziri Katambi akutana na Balozi wa China Nchini
Waziri Nanauka Ataka vijana wasikilizwe
Soma Jinsi ya Kupunguza uzito kwa siku 7 Bila Madhara
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 - Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33