Staa wa Bongo Fleva ambaye kwa sasa
anafanya kweli kimataifa, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameandika
historia kwenye Tuzo za Black Entertainment Television (BET) 2014 huku
akiwatia kiwewe mastaa wakubwa kama Cornell Iral Haynes ‘Nelly’,
Christopher Maurice ‘Chris Brown’ na wengine kibao.
TUZO YAENDA KWA DAVIDO
Tuzo hiyo haikuwa bahati kwa Diamond kwani ilikwenda kwa Davido.
Licha ya kukosa tuzo hiyo, yapo mengi ambayo Diamond ameweka historia au
rekodi katika ‘event’ huku kuunganishwa na mastaa hao ikiwa topiki
muhimu.
MCHUMBA WA CHRISS BROWN AMSHOBOKEA
Katika hali ya kushangaza, mwanamitindo maarufu Marekani ambaye ni
mchumba wa Chris Brown, Karrueche Tran alionekana kumshobokea Diamond
mara alipokutana naye uso kwa uso.
Karrueche alijikuta hajiwezi alipokuwa akimhoji Diamond ambapo moja kwa
moja alimvutia kipaza sauti na kuanza kumpiga maswali huku akionesha
kuvutiwa naye kwa muonekano aliokuwa nao.
MASTAA MACHO JUU
Ulipofika wakati wa utoaji tuzo katika kategori ya Mwanamuziki Bora
kutoka Afrika, lilipotajwa tu jina la Diamond kutoka Tanzania na wimbo
wake wa Number One RMX, mastaa kibao walionesha kushangaa na ndipo macho
yote yakahamia eneo aliokuwa amekaa.
Wengi walionekana kutoa maneno ya chinichini sambamba na kumuoneshea vidole wakionesha kumkubali kwa kutinga mjengoni hapo.
NELLY, CHRIS BROWN WAINGIWA KIWEWE
Wakati Diamond anaingia ukumbini, mastaa mbalimbali duniani walionekana
kumshangaa na kati yao alikuwa ni Nelly ambaye aliushikilia mkono wa
Diamond kwa sekunde kadhaa akitaka waendelee kupiga stori.
Kila sehemu aliyokuwa akienda, Nelly hakutaka kumuacha na alionekana
kuambatana naye kwa kumng’ang’ania mkono kila kona akipiga naye picha na
kuzunguka eneo lote wakiwa pamoja.
Naye Chris Brown ambaye aliangusha bonge la shoo alionekana kumshangaa Diamond huku akitamani kuendelea kukaa naye.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu ukumbini humo, maswali mengi yaliibuka
kuwa iweje, kwa Mtanzania kama yule kukanyaga katika mjengo mmoja na
mstaa wa dunia.
TYSON, MAYWEATHER WADUWAA
Mabondia maarufu duniani akiwemo Floyd Mayweather na Mike Tyson
walijikuta wakiduwaa kwa kumshangaa kwa kila hatua aliyokuwa anapiga.
Macho yao hayakuwa mbali naye na hata katika zulia jekundu, Maywearher,
baada ya kumaliza kupiga picha akiwa na mkewe alimfuata Diamond na
kuongea naye mawili-matatu kuonesha kukumkubali.
MASTAA KIBAO WAGOMBEA NAMBA
Wakati shoo hiyo ikiendelea baadhi ya msataa waliokuwa pembeni na
Diamond walionekana kumfagilia na hata wengine kuomba namba za simu kwa
malengo tofauti ikiwa ni pamoja na kutaka kufanya naye kolabo katika
siku za usoni.
Walionekana kuwa na furaha kwa pamoja na ikumbukwe kuwa Lupita
amejizolewa umaarufu mkubwa ambapo hata Jay-Z na Rihanna waliwahi
kuandika kupitia kurasa zao kwenye mitandao ya kijamii wakioneshwa
kumkubali kwa kazi zake.
Mastaa wengine wakubwa aliokutana nao ni pamoja na Ashanti, DJ
khalid, Jeniffer Hudson, French Montana, John Legend, Paris Hilton na
wengine kibao
HABARI NYUMA YA PAZI
Duru za kibahari zilieleza kwamba mambo yote yanayokea kwa Diamond kuna
nguvu kubwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
ambaye hivi karibuni alimkutanisha mtoto huyo wa Tandale na meneja wa
wanamuziki wakubwa duniani, Tremaine Neverson ‘Trey Songz’ na Sean
Michael Leonard Anderson ‘Big Sean’, ili kufanya nao kazi.
“Siyo jambo rahisi na bado milango itazidi kufunguka zaidi kwani JK
aliahidi kumsaidia. Kwa kuunganishwa na mastaa wakubwa duniani sasa hivi
utasikia amehamia Marekani kutusua mtonyo,” alisema mmoja wa wasanii wa
Bongo Fleva ambaye naye anafanya vizuri.
“Kuna mengi nafanya nao lakini siwezi kuwataja kwa sababu si unawajua Wabongo?
“Lakini nikidondoka tu Bongo naachia video mbili kali sana, mashabiki wangu wasikilizie.
“Kuhusu kukosa tuzo, mimi naona ni mwanzo mzuri. Inanipa hasira ya
kutengeneza muziki mzuri utakaopendwa na watu wengi duniani. Tusikate
tamaa, ni mwanzo mzuri. Pia asiyekubali kushindwa si mshindani,”
alifunguka Diamond akimshukuru Mungu kwa yote anayomtendea kila kukicha
kisha watu wanampa sapoti.