Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu, ametangaza kifo cha Mbunge wa Peramiho, Mhe. Jenista Joakim Mhagama, kilichotokea leo tarehe 11 Desemba 2025 Jijini Dodoma.
Katika taarifa hiyo, Spika Zungu amesema:
“Kwa masikitiko makubwa, naomba kutangaza kifo cha Mbunge wa Peramiho Mhe. Jenista Joakim Mhagama kilichotokea leo 11 Desemba, 2025 Jijini Dodoma. Natoa pole kwa Waheshimiwa Wabunge wote, familia ya marehemu, ndugu, jamaa na Wananchi wa Jimbo la Peramiho. Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu.”

Aidha, Ofisi ya Bunge ikishirikiana na familia ya marehemu imesema inaendelea kuandaa mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitatolewa mara zitakapokamilika.
Mhe. Jenista Mhagama, aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, amekumbukwa kama kiongozi mahiri, mchapakazi na mwenye kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
“Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina,” imehitimisha taarifa hiyo.
Jeshi la Polisi: Hakuna Maandamano Video Zinazosambaa ni za Zamani
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






