Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Bodi ya Mikopo ya Wananfunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imepanga kutoa mikopo yenye thamani ya Sh. Bilioni 450 kwa wanafunz 128,285 katika mwaka wa masomo 2019/2020.
Akizungumza na waandishi Habari katika Maonesho ya Vyuo Vikuu katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi hiyo Veneranda Malima amesema kuwa kati ya wanafunzi hao wa mwaka wa kwanza watakuwa 45,000.
Amesema mwaka wa bajeti 2018/2019 bajeti iliyokuwa imepangwa ilikuwa ni sh.Bilioni 427.7 kwa kusomesha wanafunzi 123,000, kati yao wanafunzi wa mwaka wa kwanza walikuwa 41885.
Malima amesema kuwa kuna ongezeko kubwa na kutaka wanafunzi wafuate taratibu za Uombaji wa mikopo kwa ajili ya elimu ya juu.
Amesema wako katika maonesho hayo kwa ajili ya kutoa elimu pamoja na kujibu changamoto za wanafunzi katika Uombaji wa mikopo hiyo.
Aidha amesema kwa walionufaika na mikopo urejeshaji umezidi kuongezeka na kutaka kuendelea kurejesha kwa ajili ya kunufaisha wengine.
Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Veneranda Malima akizungumza na waandishi habari katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wakipata maelezo kwa Afisa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kuhusiana na Uombaji wa mikopo ya elimu ya Juu katika Bodi hiyo katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wakipata maelezo kutoka Kwa maafisa Bodi katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2l96dxK
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33









