Akikabidhi msaada huo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Ndani wa NMB, Juma Kimori, alibainisha kwamba thamani ya vitanda vyote ni Sh. Milioni 45 huku akifafanua kuwa kitanda kimoja cha ICU ya watoto kimegharimu Sh. Milioni 7.5 na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali kuboresha sekta ya afya.
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Zuhura Mawona, aliishukuru na kuipongeza NMB kwa msaada huo na kuiomba iendelee kutoa msaada zaidi kwa ajili ya chumba hicho maalum kwa watoto.
“Tulipeleka maombi NMB na wametujibu hatuchoki, tunaendelea kuwaomba mtushike tena mkono, maana mahitaji ya vitanda katika chumba hicho muhimu cha kuokoa maisha ya watoto ni mkubwa, bado tunahitaji vingine saba mkiguswa tena mtukumbuke.
“Kabla ya wodi hii kuanza watoto walikuwa wanachanganywa kwenye ICU za wakubwa na kule vitanda sio sawa na hivi tulivyopokea vya NMB hata sisi wahudumu hatupati tabu sana kuvinyanyua wala mgonjwa haumii kila kitu kinasetiwa kwenye umeme asanteni sana NMB,” alisema Mawona aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Hospitali ya Taifa Muhimbili.#NMBKaribuYako
Mkaguzi wa Mahesabu ya Ndani wa Benki ya NMB, Peter Kimori akimkabidhi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto; Mh. Ummy Mwalimu msaada wa vitanda 15 kwa ajili ya chumba cha watoto wagonjwa waliopo kwenye uangalizi maalum(ICU) katika hospitali za Muhimbili na Mloganzila za jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto; Mh. Ummy Mwalimu na Mkaguzi wa Mahesabu ya Ndani wa Benki ya NMB, Juma Komori wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao kutoka hospitali za Muhimbili na Mloganzila.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2qXNrgk
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






