Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Singida, Salum Mahami, akiongoza kuomba dua katika Swala ya Eid Al-Haji iliyofanyika Viwanja vya Shule ya Msingi Sumaye mkoani hapa leo.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Singida, Salum Mahami (kulia), akiongoza kuomba dua katika Swala ya Eid Al-Haji iliyofanyika Viwanja vya Shule ya Msingi Sumaye mkoani hapa leo. Kushoto ni Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata) Mkoa wa Singida, Burhan Mlau.
Sheikh Shabani Mkanga akisoma hutuba katika swala hiyo.
Waumini wa dini ya kiislamu wa mkoa wa Singida wakishiriki swala hiyo.
Waumini wa dini ya kiislamu wa mkoa wa Singida wakishiriki swala hiyo.
Wanawake wa Kiislamu wakiwa kwenye swala hiyo.
Watoto na wakishiriki na wazazi wao katika swala hiyo.
Dua ikifanyika.
swala ya Eid -Al- Haji baada ya kumalizika
Na Dotto Mwaibale, Singida
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Singida limetoa pole kwa Rais Dkt.John Magufuli kufuatia msiba wa watu 71 waliofariki kwa ajali ya kuungua moto mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki.
Pole hiyo kwa Rais imetolewa na Katibu wa Bakwata Mkoa wa Singida, Burhan Mlau katika swala ya Eid- Al-Haji iliyofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Sumaye mkoani hapa.
“Tunampa pole Rais wetu kwa msiba huu mkubwa tulioupata pamoja na wafiwa na tunawaombea majeruhi wote wapate nafuu waweze kurejea katika shughuli za ujenzi wa taifa” alisema Mlau.
Mbali ya Rais Magufuli wengine waliopewa
pole hiyo ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Steven Kebwe pamoja na wananchi wote wa mkoa huo na kuwa Taifa limepoteza nguvu kazi kubwa.
Katika swala hiyo Mlau aliwataka Waislamu wa mkoa huo kuwa kitu kimoja na kuondoa utengano kupitia taasisi zao mbalimbali badala ya kutengana.
“Nawaombeni ndugu zangu waislamu tuendelee kushikamana na kupendana kupitia taasisi zetu jambo ambalo litadumisha uislam wetu na kumpendeza mwenyezi mungu” alisisitiza Mlau.
Katika kusherehekea sikukuu hiyo Mlau aliwaomba waislam wa mkoa huo kusherehekea kwa utulivu na amani huku wakiwangalia watoto wao kwa ukaribu.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2YYsxbU
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33















