Zipo nyingi sana, lakini hapa nitakupa dalili ambazo ukiona mwanamke wako anazo ujue hana penzi la moyoni.
ANAKUTEKA
Mwanamke
ana haki ya kudeka kwa mwanaume wake, lakini siyo kwa nia nyingine
yoyote zaidi ya kunakshi penzi. Huyu hana nia hiyo, anadeka kwa ajili ya
kukupagawisha kimahaba ili aweze kuzishika hisia zako sawasawa.
Mchunguze
vizuri, utagundua kwamba hata sauti yake anayoitumia kuzungumza na wewe
siyo anayotumia akiwa na shoga zake. Anailegeza kwa kuiremba kwa kila
hali.
Anataka
kukupagawisha. Hiyo ndiyo nia yake, kukupagawisha sana maana yake
hutapindua na hutakuwa na wazo la kuwa na mtu mwingine zaidi yake.
ANAPENDA FEDHA
Ni kawaida mwanamke kumuomba fedha mpenzi wake, lakini huyu asiye na mapenzi ya kweli, huwaza fedha mara zote.
Hata kama utazungumza kuhusu kutoka naye katika matembezi, bado ataulizia kuhusu dau lake.
Ana
mahitaji mengi. Mwanamke wa aina hii, ukitoka naye nje ya mji au kulala
naye hotelini, asubuhi atataka chake! Jiulize ni mpenzi wako au
anajiuza? Mbaya zaidi, hata kama utakuwa mgonjwa na amekuja kukutazama
siyo ajabu kabisa kukuomba fedha, akiwa na tabia hii ujue hana mapenzi,
anataka kukutumia.
HANA HESHIMA
Kwa
kuwa hakupendi na wala hafikirii kuwa na wewe katika ndoa, sifa za
uanamke hatakuwa nazo. Inawezekana kabisa anazifahamu vizuri sana sifa
hizo, lakini hana muda nazo.
Hasikii ukimwambia kitu, mjeuri na wala haheshimu kauli zako.
Kama
mpenzi wako, ambaye una malengo naye ya baadaye, una haki ya kumzuia
aina fulani ya mavazi, kampani au tabia ambazo huzipendi.
Kwa mwanamke wa aina hii, kumwambia ni sawa na kumruhusu! Mwanamke huyu, neno heshima ni msamiati mgumu sana kwake.
Unajua kwa nini? Kwa sababu hakupendi
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33





