Mwimbaji staa wa bongofleva Ali Kiba ameungana na mastaa wengine kama Diamond Platnumz, Wema Sepetu, Steve Nyerere, Aunty Ezekiel, Ray ‘Vicent Kigosi’ na wengine kuiunga mkono CCM na mgombea wake Urais ambaye ni Dr. John Pombe Magufuli.
Pamoja na kwamba Ali Kiba ameonekana kwenye headlines za kampeni za CCM, hakuwahi kuandika au kupost chochote kwenye kurasa zake kuhusu kiongozi gani anaeona ni sahihi kwake ila sasa ndio amefanya maamuzi hayo kwa mara ya kwanza.
Credit: Millardayo