
Jana Usiku Desemba 07 imeandikwa tena Historia kwa wapenzi wa Burudani ndani ya Manispaa ya Bukoba na Viunga vyake, katika Tamasha kubwa linaloandaliwa na Kituo cha Redio Kasibante Fm, kilichopo Mkoani Kagera, ambalo hufanyika Desemba kila Mwaka, ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kuanzishwa kwa kituo hicho.
Burudani hiyo ya kiwango cha aina yake imefanyika ndani ya Kumbi za Lina’s Night Club kwa kuwakutanisha mamia ya wapenzi wa Burudani hususani wasikilizaji wa kituo hicho pendwa, pamoja na wasanii nguli wa muziki wa Dansi na Bongo Fravoul.
Burudani ilianza majira ya saa tatu usiku kwa kutanguliwa na wasanii wa nyumbani (wenyeji) akiwemo msanii anaefanya vizuri katika kiwanda cha Bongo fravoul HarmyD planet, na kisha baadae kutoka Jijini Dar es salaam orodha ilifunguliwa na Baddest 47 mzee wa nikagongee.
Shangwe zilidishwa na kunogeshwa zaidi na Baba na mwana Nguza Viking na Papii Kocha, walioonekana kuuteka usiku wa burudani kwa kuwanyanyua mamia ya wakazi wa Kagera kwenye viti vyao na kuimba nao nyimbo zao zilizowahi kutamba Salima, Fanta, Sea na nyingine.















.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2qAJpKC
via






