VETA yatoa gawio la Shilingi Bilioni 1 kwa Serikali

6 years ago80 Views

 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akipokea mfano wa hundi ya Shilingi bilioni moja kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Ndg. Peter Maduki (kushoto) ikiwa ni gawio la VETA kwa Serikali katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma leo tarehe 12 Desemba 2019. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt. Pancras Bujulu. Wengine katika picha ni Msajili Hazina, Athumani Mbuttuka na Naibu Katibu Mkuu, Adolf  Ndunguru.
Watendaji Wakuu wa VETA wakisikiliza nasaha kutoka Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango wakati wa hafla ya kuwasilisha gawio kwa Serikali iliyofanyika jijini Dodoma leo, tarehe 12 Desemba 2019. Katika hafla hiyo VETA imetoa gawio la Shilingi Bilioni Moja. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Ndg. Peter Maduki, Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt. Pancras Bujulu (katikati) na Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa VETA Ndg. Anthony Kasore (kushoto).

from MICHUZI BLOG https://ift.tt/38sTj1P
via

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.