
KATIKA kukuza sekta ya elimu katika Wilaya ya Kongwa, Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe Deo Ndejembi amekabidhi mabati, mbao na mawadati yenye thamani ya Sh Milioni 25 kwa Shule za Msingi na Sekondari wilayani humo.
Vifaa hivyo vimetolewa kwa shule sita za wilaya ya Kongwa na Benki ya NMB ambapo wamemkabidhi DC Ndejembi huku wakisema wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuihudumia jamii lengo likiwa ni kumuunga mkono Rais Dk John Magufuli katika kuwatumikia watanzania.
Akipokea vifaa hivyo kutoka kwa Meneja wa NMB kanda ya kati Nsolo Mlozi, DC Ndejembi amesema vifaa hivyo vitatumika kumaliza changamoto iliyokuepo na kuahidi kuhakikisha anasimamia kila Shule kupata mgawo kwa unaotakiwa kwa usawa.
Amesema Wilaya ya Kongwa imekua ikifanya vizuri kwenye sekta ya elimu ambapo mwaka huu wanafunzi 5000 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2020 huku akijinasibu pia kufanya vizuri kwa matokeo ya kidato cha nne.
” Tunawapongeza NMB hakika mmetushika mkono, tuna uhaba wa vyumba 39 vya madarasa lakini kwa sapoti yenu hii ya mabati, mbao na madawati hakika tutapunguza changamoto iliyopo.
Milioni 25 mngeweza kuzifanyia jambo lolote lakini mmeamua kumuunga mkono Rais wetu Dk Magufuli kwa kurudisha mchango wenu kwenye jamii hasa kwenye sekta ya elimu. Niwaahidi kusimamia vifaa hivi katika kuzifikia Shule zote zilizolengwa na zitumike vizuri,” Amesema DC Ndejembi.
Amezitaka Taasisi nyingine za kifedha kurudisha mchango wao kwenye jamii hasa katika sekta ya elimu, afya na majanga ambapo huwalenga moja kwa moja wananchi wetu ambao kimsingi ndio wateja wa Benki hizo.
Kwa upande wake Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi amesema kila mwaka wamekua wakitenga kiasi cha fedha kwenye faida yao kwa ajili ya kurudisha mchango wao kwenye jamii na mwaka huu wametenga kiasi cha Sh Bilioni moja ambazo watazipeleka kwenye sekta mbalimbali.
Amesema Wilaya ya Kongwa imenufaika na vifaa hivyo kutokana pia na kuwa na idadi kubwa ya watu wanaotumia huduma ya benki hiyo hivyo wakaona ni vema kutenga kiasi cha Sh Milioni 25 kwa ajili ya elimu ndani ya wilayani humo.
” NMB tumekua na kawaida ya kutoa mchango wetu kwenye jamii katika nyanja tofauti ikiwemo Elimu, Afya, Majanga na Elimu ya Fedha kwa wanafunzi. Hivyo niwasihi wanafunzi kusoma kwa bidii ili kumtia moyo Mhe Rais Magufuli ambaye ama kwa hakika ameleta ukombozi kwenye sekta hii kwa kutoa elimu bila malipo.
Niwaombe wazazi na taasisi nyingine pia kuwa na uchungu na elimu kwa kutoa michango ili kupunguza changamoto ambazo zimekua zikijitokeza,” Amesema Mlozi.
Kiasi hicho cha Sh 25 Milioni kimeenda kwa Shule sita ambapo Shule ya Msingi Kibaigwa imepata mabati ya Sh Milioni Tano, Shule ya Msingi Miembeni imepata madawati ya Sh Milioni Tano, Shule ya Msingi Chinangali imepata Sh Milioni Tano, Shule ya Msingi Muungano imepata Milioni 2.5
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36QsgMl
via






