TAARIFA KWA UMMA KUHUSIANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA.

6 years ago114 Views

Kutokana na uwepo wa mvua kubwa zinazoendelea kunyesha karibu mikoa yote hapa  chini na mvua kusababisha mito kujaa sana na maji kuwa na kasi kubwa. Hivyo baadhi ya sehemu maji hufurika na kufunika madaraja na makaravati.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linawatahadharisha wananchi kutothubutu kujaribu kuvuka kwenye madaraja au makaravati yaliyofunikwa na maji, kuna uwezekano mkubwa daraja au karavati kusombwa na maji. Aidha madereva wasijaribu kuvusha vyombo wanavyoendesha maana ni hatari kufanya hivyo.

Kuvuka maeneo kama hayo kunaweza kuleta maafa makubwa kwa jamii ikiwemo kupoteza maisha kwa kusombwa na maji. Hivyo wasubiri mpaka maji yatakapopungua kiasi kwamba daraja au karavati vinaonekana vizuri na ni salama kuvuka, pia watu wasitembee kwenye kingo za mito, maana kingo za mito huwa dhaifu kutokana na ardhi
kujaa maji.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limejipanga na liko imara kuhakikisha linatoa huduma bora, sahihi na kwa wakati. Hivyo wananchi mnapoona janga lolote tafadhali toeni taarifa mapema kwa kupiga namba ya dharura 114.
Imetolewa na:

KITENGO CHA HABARI, UHUSIANO NA ELIMU KWA UMMA
MAKAO MAKUU
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

from MICHUZI BLOG https://ift.tt/38WTSkO
via

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.