Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii Amani, Tanga
Katika kuendelea kuwepo kwa maji ya uhakika na yenye usalama hakuna budi jamii kuhifadhi vyanzo vya maji wanavyozunguka kwa kuendesha shughuli za kilimo zisizo na madhara katika vyanzo hivyo.
Vyanzo ya maji vikihifadhiwa kwa katika sekta ya kilimo kwa kupanda mazao ambayo hayana madhara katika utiririshaji maji mamlaka husika kupunguza gharama za kutibu maji wakati wa usambazaji wa maji hayo kwa wananchi.
Mkoa wa Tanga kwa wananchi wanaozunguka vyanzo vya maji wameunda Umoja wa Kilimo na Uhifadhi wa Mazingira Kihuhwizigi (Uwamasiki) ambao wamekuwa wakihifadhi vyanzo vya maji na kufanya mamlaka ya Maji Safi na Mazingira jiji la Tanga Tanga Uwasa) kuunga mkono jitithada za umoja huo.
Kutokana na Mamlaka ya Tanga kuwa umoja wenye nguvu katika uhifadhi vyanzo vya maji Bonde la Wami/Ruvu imepeleka jumuiya za Watumia Maji katika vyanzo vya bonde hilo kujifanza katika umoja wa Kilimo na Uhifadhi wa Mazingira (Uwamasiki) ili kuleta chachu kuongeza mbinu katika uhifadhi wa vyanzo vya maji.
Akizungumza wakati wa ziara ya Jumuiya ya Watumia Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Jamii na Mahusiano wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu Horold Kayoza amesema kuwa wamepeleka jumuiya hizo kwenda Tanga kwenda kujifunza namna Umoja wa Kilimo na Uhifadhi wa Mazingira (Kihuhwi) inavyolinda vyanzo vya maji kwa kuendesha shughuli mbalimbali katika vyanzo hivyo ikiwemo kilimo.
Kayoza amesema baada ya kutoka Tanga nia ni kuona jumuiya ya watumia maji wanakwenda na kasi ya kuweka mikakati ya kuhifadhi vyanzo vya maji kwa kushirikisha wadau wote kwa kutumia elimu walioipata katika ziara ya Mkoa wa Tanga.
Aidha amesema kuwa mazingira ya vynzo vya maji katika mkoa wa Tanga havina tofauti na Mikoa ya Morogoro na Pwani hivyo wanajumuiya ya watumiaji katika Bonde la Wami/Ruvu watatumia mbinu mbalimbali walizozipata katika ziara ya Tanga.
Nae Afisa Udhibiti Ubora wa Huduma na Mratibu wa Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira jiji la Tanga (Tanga-Uwasa) Ramadhan Nyambuka amesema kuwa kutokana na Umoja wa Wakulima na Uhifadhi wa Mazingira (KIHUHWIZIGI) kuhifadhi vyanzo vya maji kumeleta matokeo chanya kwa mamlaka kupunguza gharama za kutibu maji.
Amesema kuwa wakati umoja huo ukiwa haujaanzishwa walikuwa wanatumia gharama kubwa ya kutibu maji lakini kuanzishwa kwa umoja huo Tanga-Uwasa limeendelea kupunguza gharama hizo ikiwa ni kuunga mkono kwa ufadhili wa miradi kwenye umoja ili waendelee kutunza vyanzo vya maji.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima na Uhifadhi wa Mazingira KIHUHWIZIGI , Twaha Mbaruku amesema kuwa umoja umesimama vizuri kutokana na kila mmoja kujua umuhimu wa kuhifadhi vyanzo vya maji.

from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Myqd8a
via









