UMESIKIA walichokutana nacho Hugo Lloris, Harry Kane? Iko hivi Tottenham Hotspur waliendesha zoezi la kuwapata wachezaji wao bora kwa nafasi mbalimbali kwa kipindi cha muongo mmoja (miaka 10).
Sasa katika eneo la golikipa nafasi hiyo ilikua ikishindaniwa na Gomes, Brad Friedel na Hugo Lloris. Sass kwa kuwa Friedel aliwahi kucheza Liverpool mwaka 1997-2000 basi mashabiki wa Liverpool wakaingilia box la kura huko Twitter matokeo yake Friedel akashinda.
Ubabe ulikua kwenye tuzo ya mshambuliaji bora ambapo ilikua ikiwaniwa na Jermaine Defoe, Harry Kane na Peter Crouch.
Mwanzo Kane alikua akiongoza kwa asilimia 90 lakini Liverpool walivyoweka post hiyo Twitter upepo ukabadilika Crouch ambaye alipita Anfield mwaka 2005-2008 akashinda na kuwa mshambuliaji bora wa Spurs licha ya Crouch mwenyewe kumuombea kura Kane.
UKUMBUSHO: Misimu miwili nyuma Liverpool walihamasishana kumpigia kura Lucas Leiva kuwa mchezaji bora wa Lazio. Kumbuka Leiva aliwahi kucheza Liverpool.
Yaani wasije wakajichanganya tuzo ya mchezaji bora wa Dunia iwe inapigiwa kura online na mshindi apatikane kwa kura za mashabiki online Liverpool itashinda kila mwaka.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2F8eeK7
via



