Mh Mavunde alitumia fursa hiyo kuwapa pole wafanyabiashara hao kwa majanga hayo ya moto na upotevu mkubwa wa bidhaa zao na kuwachangia bati 52 zenye thamani ya Tsh 1,200,000 ili kurejesha vibanda vyao katika hali ya Kawaida.
Naye Mkuu wa Wilaya wa Dodoma Mh Patrobas Katambi amewataka wafanyabiashara hao kuhakikisha wanapata taarifa za tukio la moto kutoka mamlaka husika kwa ajili ya uthibitisho kwenda Taasisi za fedha ambazo wafanyabiashara wengi wengi wamekopa na kutumia nafasi hiyo hiyo kuwaagiza TANESCO kutoa elimu ya masuala ya umeme na kuwaunganishia umeme wafanyabiashara hao kwa utaratibu,huku Jeshi la ZIMAMOTO likiagizwa kufika na kutoa ushauri juu ya ujenzi wa vibanda hivyo.
Wakati huo huo Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Ndg Godwin Kunambi amewahakikishia wafanyabiashara hao kwamba Jiji la Dodoma litaboresha eneo la Soko la Sabasaba na kujenga vibanda vipya 400 vya kisasa ili soko hilo liendane na hadhi ya Jiji.
Akishukuru kwa niaba,Makamu Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao Bi. Eliza Siame amewashukuru viongozi hao kwa kufika eneo la tukio na kuwapa pole pamoja na mchango wa bati 52 ambazo zitasaidia kurejesha vibanda hivyo katika hali yake ya kawaida.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2QlCgrL
via




