RC SENYAMULE AFURAHISHWA NA UWEKEZAJI WA KIWANDA KIKUBWA CHA SARUJI DODOMA,JIONEE VIDEO HII

Admin Updates2 years ago6 Views

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule ameshuhudia utiaji saini mkataba wa makubaliano ya ujenzi wa kiwanda kikubwa cha uzalishaji saruji kinachotarajiwa kujengwa wilayani Kongwa jijini Dodoma.


Makubaliano hayo ya ujenzi wa kiwanda hicho kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani milioni moja kwa mwaka na kuanza kuajiri wafanyakazi 5000 yamesainiwa na viongozi wa kampuni zilizoingia ubia ambapo kwa upande wa Tanzania alisaini Mkurugenzi wa Kampuni ya Alotab & Block BB, Abdul Hillary Ally (kushoto) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Libyan Petrolium ya Libya, Dmjed Rajab (kulia).

Hafla hiyo imefanyika Machi 17, 2023 mbele ya wajumbe wa Baraza la Ushauri Mkoa wa Dodoma (RCC) jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Alotab & Block BB, Abdul Hillary Ally (kushoto) akitia saini mkataba huo.
Wakibadilishana hati
Mkurugenzi wa Kampuni ya Alotab & Block BB, Abdul Hillary Ally akitoa neno la shukrani kwa serikali.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Libyan Petrolium ya Libya, Dmjed Rajab akitoa neno la shukrani kwa serikali.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule  akielezea furaha yake kwa kampuni hizo kuamua kuwekeza kiwanda hicho Dodoma na kwamba kitasaidia kuleta ajira na kuinua pato la mkoa huo na Taifa kwa ujumla.

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, wabia hao wakielezea sababu zilizowafanya wawekeze Dodoma…

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.