Mwanamuziki Aslay Awachana Mastaa “Kuimba Amapiano…Asema ni ……”

Admin Updates1 year ago7 Views

 

Msanii wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka amesema kuwa yeye hawezi kuimba muziki wa Amapiano kutoka Afrika Kusini kama ambavyo wasanii wengi wa Bongo wamekuwa wakifanya.

Aslay amesema hayo wakati akihojiwa na EA Radio kufuatia sintofahamu iliyoibuka mitandaoni baada ya idadi kubwa ya mastaa Bongo kuhamia kufanya muziki huo na kuonekana kama wanataka kuutelekeza muziki wao wa Bongo Fleva.

“Amapiano sio muziki mbaya kusema tuuponde, hapana ni muziki mzuri hata mimi ni shabiki sana wa Amapiano na ninasikiliza, lakini imefufuliza sana mpaka unahisi tupo Sauzi.

“Ninawashauri kaka zangu ambao tunaamini wako hapo juu wanapigiana kelele, wasiisahau Bongo Fleva yetu, wakifanya Amapiano wafanye na Bongo Fleva hata mbili tatu.

“Mimi kusema kweli Amapiano siiwezi, na sidhani kama nitakuja kufanya Amapiano kwa sababu mimi ni Bongo Fleva.

“Nina miaka zaidi ya 10 kwenye tasnia hii, kuna kitu ambacho ninakitengeneza ili hata wasanii wadogo zangu watakaokuja nyuma nyuma yangu waseme miongoni mwa watu waliofanya kazi kubwa ya kuipandishq Bongofleva na mimi nimo.

“Mimi nitaendelea kubakia hapa kwenye Bongofleva kwa sababu hata nikiimba muziki kama Amapiano ninaona kama ninajishobokesha sehemu ambazo sizo uongo dhambi,” amesema Aslay.

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.