Mikopo Kausha Damu Chanzo Ndoa Nyingi Kuvunjika Mitaani,Soma hii taarifa

Admin Updates1 year ago6 Views

Mikopo umiza inayotolewa na watu binafsi mitaani imetajwa kuwa chanzo Cha ndoa nyingi kuwa hatarini kuvunjika kutokana na baadhi ya Wanawake kuweka dhamana vitu vya ndani ikiwemo hati za Nyumba na vinginevyo
Wakizungumza Wanawake wa Manispaa ya Shinyanga wamesema changamoto kubwa ni Mikopo umiza wanayochukua mitaani ambayo inasababisha wengi kuingia kwenye matatizo ya Kifamilia
Kwa Upande wake,Mbunge Viti maalum Shinyanga Salome Makamba wakati akiwatembelea Wakina Mama hao katika Maeneo Yao amesema wengi wamekua wakifuata mikopo hiyo kwakua ni nafuu Lakini huishia vilio
Nae Mkazi Wa Manispaa Shinyanga Mariam Senkondo amesema Mikopo Umiza imekua Janga Kubwa Kwa Wanawake kutokana na wengi wao kushindwa kulipa marejesho na familia kuingia hatiani
“jamani Wakina mama tuna wakati mgumu sana tunapenda mikopo Ili tufanye biashara Lakini inatuumiza wengine wanaita Kausha damu Sasa ukifikiria kwenda Benki masharti ni magumu zaidi ni Bora tufie hukuhuku”
Aidha,Wanawake hao wameiomba Serikali kuangalia pamoja na kuwadhibiti watu wanaofanya biashara ya kukopesha fedha na kutoza Riba kubwa ambayo imekua kama njia ya kuwakandamiza wenye kipato Cha chini .

 

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.