“Mimi nilikuwa nimenunua [ndege] kubwa ya kwangu ila wakaniletea ujanja wakaniingiza mjini kidogo wakanipiga kama bilioni 4 na kitu.” alisema.
Muhtasari
• “Mpaka kufikia mwaka huu nilikuwa nimeshapanga kwamba sitakuwa tena nasafiria ndege za biashara,” alisema.
• “Mpaka kufikia mwaka huu nilikuwa nimeshapanga kwamba sitakuwa tena nasafiria ndege za biashara,” alisema Diamond.
Msanii Diamond ambaye amekuwa akizunguka mataifa mbali mbali kwa kutumia ndege ya kibinafsi kwa mara ya kwanza amefufua uvumi kuhusu umiliki wa ndege yake ya kibinafsi ambao ulizagaa mwaka jana.
Diamond alikuwa anazungumza na waandishi wa habari baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kahama kwa ajili ya tamasha la Wasafi Festival ambapo aliulizwa kuhusu uwepo wa ndege yake ya kibinafsi kama alivyowaaminisha mashabiki wake mwaka jana.
Msanii huyo alifichua kwamba alipigwa usinga wa kichawi na kuingizwa mjini na watapeli ambao walimuahidi ndege na baada ya kuwapokeza hela Zaidi ya bilioni 4 za kitanzania, wakachimba mitini na kusangarai.
Hata hivyo, msanii huyo aliweka wazi kwamba mamlaka husika katika serikali ya Tanzania inajua hilo na inaendelea kufuatilia ili bilioni zake 4 zipate kurejea au apate ndege yake ya kibinafsi.
“Suala liko lakini [watapeli] wametuchelewesha sana. Sisi tulitakiwa tuwe na ndege yetu zamani sana tuwe tunazunguka nayo. Mpaka kufikia mwaka huu nilikuwa nimeshapanga kwamba sitakuwa tena nasafiria ndege za biashara, nilikuwa nataka nisafiri na ndege yangu tu,” alisema.
“Mimi nilikuwa nimenunua [ndege] kubwa ya kwangu ila wakaniletea ujanja wakaniingiza mjini kidogo wakanipiga kama bilioni 4 na kitu. Polisi wanafahamu na inaendelea kufuatiliwa na serikali wananisaidia kuona haki yangu naipata aje,” aliongeza.
Msanii huyo alisema kwamba ameshaanza kurudishiwa kidogo hela hizo na anaamini mwisho wa siku atapokea hela zake zote ili kuendelea na ndoto yake ya kumiliki ndege ambayo alisema kuwa haitakuwa yake pekee bali pia watu wengine watakuwa na uwezo wa kuikodisha na kuitumia vile vile.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







