KESI YA KIFO CHA MSANII KANUMBA YAIBUA SURA MPYA!

Admin Updates10 years ago5 Views

Baada ya kimya cha muda mrefu, imefichuka
kwamba kesi ya kuuawa kwa aliyekuwa staa mkubwa wa sinema za Kibongo,
marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ imechukua sura mpya baada ya
kuanza kusikilizwa kimyakimya, Ijumaa Wikienda limenasa kinachoendelea.


Staa wa sinema za Kibongo, Lulu Elizabeth Michael, ‘Lulu”.


WATU WANATAKA KUJUA KINACHOENDELEA
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba watu wengi wana kiu ya kujua
kinachoendelea katika kesi hiyo ambapo ilidaiwa kwamba imehamishwa eneo
la wazi (open) na kusikilizwa kimyakimya katika Mahakama Kuu ya
Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, huku usikilizwaji wa kesi hiyo ukiwa
tofauti kama ilivyozoeleka.
Kwa mujibu wa shushushu wetu anayependa kufuatilia maisha ya mastaa
wa tasnia tofautitofauti Bongo ndani ya mahakama hiyo, chombo hicho cha
kusimamia sheria kimeamua kubadili aina ya usikilizaji wa kesi hiyo.



Wakili maarufu Bongo anayemtetea ‘Lulu’, Peter Kibatala.


YAHAMISHIWA BARAZA LA KESI ZA MAUAJI
Habari zilieleza kwamba, kwa sasa kesi hiyo itakuwa ikisikilizwa kwenye
kikao cha baraza la kusikiliza kesi za mauaji kwenye mahakama hiyo, kwa
lugha ya kigeni kinaitwa High Court Murder Session.
“Kama ukienda pale mahakamani ili kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo,
huwezi kufanikiwa kupata chochote kwa sababu ipo kwenye baraza la
kusikiliza kesi za mauaji yaani High Court Murder Session ambalo huwa
linasikiliza kesi kimyakimya tofauti na kesi nyingine zinazosikilizwa
kwenye kizimba,” kilisema chanzo chetu hicho.
ETI LULU HAJUI KINACHOENDELEA
Uchunguzi wetu ulibaini kwamba wakati hayo yakiendelea kortini hapo,
aliyekuwa mwandani wa Kanumba aliyekuwa naye chumbani siku ya kifo,
Elizabeth Michael ‘Lulu’ hajui chochote kinachoendelea na wala hajaitwa
mahakamani.


Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.

“Tangu imeanza kusikilizwa hakuna siku Lulu ameitwa na sidhani kama anajua kinachoendelea.
“Labda anayejua kinachoendelea ni mama Kanumba (Flora Mtegoa) ambaye
hupenda kuulizia kuhusu hatima ya mwanaye,” kilisema chanzo hicho.
WAKILI KIBATALA ANASEMAJE?
Baada ya kujikusanyia data hizo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta wakili
maarufu Bongo anayemtetea Lulu, Peter Kibatala ili kupata ufafanuzi wa
aina hiyo ya usikilizwaji wa kesi ya mteja wake ambapo alifichua siri
hiyo juu ya kesi ya kifo cha Kanumba.
Wakili Kibatala alikiri kwamba kesi ya kifo cha Kanumba ambayo Lulu
ni mshitakiwa wa kwanza akituhumiwa kuua bila kukusudia, imebadilishwa
aina ya uitwaji huku akigoma kuingia kiundani kwani bado kesi hiyo ni
mbichi na hairuhusiwi kwa wakili kuzungumza nje ya mahakama.


Aliyekuwa staa mkubwa wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ enzi za uhai wake.

“Ni kweli inaitwa hivyo, huyo aliyekueleza hajakosea na tunategemea
mwezi huu wa nane kikao cha baraza hilo la usikilizaji kitaendelea
lakini nisingependa kuongea sana kwani mimi siyo msemaji wa Lulu bali ni
wakili na si maadili ya kazi yangu kuzungumza nje ya mahakama. Hata
Lulu haruhusiwi kuzungumza chochote nje ya mahakama,” alisema Kibatala
aliyewahi kuwa wakili wa mwigizaji Kajala Masanja na mwanahip-hop,
Waziri Makuto ‘Lord Eyez’.
TUMGEUKIE LULU
Mwanahabari wetu alipomtafuta Lulu ili kujua kama anajua chochote juu ya
kesi hiyo, mkali huyo wa sinema za Kibongo aligoma kuzungumza chochote
kama aliyoelekezwa na wakili wake, Kibatala.
TUJIKUMBUSHE
Kanumba aliyewatoa mastaa wengi wa filamu unaowaona kwa sasa, alifariki
dunia April 7, 2012 nyumbani kwake, Vatican-Sinza jijini Dar. Kifo cha
Kanumba kilidaiwa kwamba kilitokana na kuangukia sehemu ya nyuma ya
kichwa ambapo alipata mtikisiko wa ubongo kisha kuzikwa kwenye Makaburi
ya Kinondoni, Dar.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.