Wema Sepetu na Van Vicker wakiwa kwenye pozi.
Habari ya mjini! Gumzo katika ulimwengu wa mastaa Bongo ni kitendo cha
mkali wa muziki wa Kizazi Kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
kuendelea kujiachia na staa wa mrembo mwenye maskani yake nchini Uganda
na Afrika Kusini ‘Sauz’, msanii Zarinah Hassan ‘Zari’ au ‘The Boss Lady’
huku aliyekuwa ‘kiburudisho’ wa jamaa huyo, Wema Isaac Sepetu
‘Beautiful Onyinye’ akijibu mapigo kwa kumnasa mwigizaji Joseph Van
Vicker wa Ghana, Ijumaa lina sarakasi nzima.
WEMA ATIMKIA GHANA
Wakati Diamond akitimkia Marekani kwenda kutumbuiza kwenye sherehe za 53
za Uhuru wa Tanganyika kwa Wabongo waishio nchini humo (Diaspora),
Desemba 9, mwaka huu, Wema yeye alitimkia kwenye Mji Mkuu wa Ghana
jijini Accra kuungana na Van Vicker kwa ajili ya ‘projekti’ kama
ilivyokuwa kwa Diamond na Zari.
Habari za uhakika zilizothibitishwa na
Wema mwenyewe zilieleza kwamba yupo nchini humo kwa ajili ya kurekodi
filamu huku wawili hao wakiwa ndiyo wahusika wakuu.
PICHA ZA MAHABA NIUE
Mapema Jumanne iliyopita, picha za mahaba niue za mastaa hao zilianza
kuvuja kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii huku kila mmoja akimsifia
mwenzake kuwa ni mkali.
ANAMLIPIZA DIAMOND?
“Hakuna, hayo ni mambo ya kizamani, mbona ishu ilikuwepo hata kabla ya
kummwaga Diamond? Unajua hizi timu ndiyo zinakuza mambo tu lakini
hawayakuzi kwa ubaya, ni namna walivyo na mapenzi na msanii wao.”
TEAM WEMA VICHEKO
Katika hali ya kushtua, ghafla wafuasi wa Wema (Team Wema) waliokuwa
wamezimwa na wale wa Diamond (Team Diamond) katika mitandao ya kijamii
waliibuka upya.
Safari hii walikuwa wakiachia vicheko na kujisifia kwamba wao ni muziki mnene hivyo hawawezi kushindana na watoto wadogo.
“Huyo bibi bomba (Zari) si lolote. Cheki
Madam (Wema) kavuka mipaka hadi Afrika Magharibi. Mtangoja sana. Sasa ni
taifa kwa taifa hadi kieleweke,” ilisomeka sehemu ya maoni ya Team Wema
kwenye Instagram na kupata dolegumba (likes) nyingi.

TEAM DIAMOND NAO
Kwa upande wao, Team Diamond nao walikuja juu na kuwapa makavu Team Wema
kuwa watangoja sana kwani tayari jamaa siyo wa Afrika tena bali duniani
kote.
VAN VICKER NI NANI?
Van Vicker amezaliwa mwaka 1977 ambapo ameoa na amejaliwa kuwa na watoto wanne.
Ni mwigizaji mkubwa barani hasa Afrika Magharibi akiwa amejijengea jina
katika tasnia ya filamu nchini Ghana ya Ghollywood na Nigeria huko
Nollywood akiwa ni mkurugenzi wa kampuni kubwa ya kuzalisha sinema ya
Sky + Orange Productions.
AMEIGIZA SINEMA GANI?
Baadhi ya filamu alizocheza ni pamoja na Divine Love, Neat Job, Friday
Night, The Hands of Time, One Night in Vegas, Total Love, When One Door
Closes, Amina, Unstopable na nyingine kibao.
SINEMA ALIZOIGIZA WEMA
Akiwa anamiliki kampuni yake ya kuzalisha sinema ya Endless Fame
Productions, baadhi ya filamu alizoigiza Wema ni pamoja na Point of no
Return, Red Valentine, Family Tears, The Super Star, House Boy, Crazy
Tenant, Basilisa, Lerato, The Diary, Tafrani, Sakata, White Maria na
nyingine.