MAMAA:MWIGIZAJI ‘RAY’ SASA KWENYE ISHU YA UTAPELI, CHEKI ALICHOMFANYIA JOHARI

Admin Updates10 years ago5 Views


Gazeti
la udaku la KIU, limeripoti kuwa hali ndani ya kampuni ya RJ inaendelea
kutokuwa shwari kwa kile kinachodaiwa kuwa kuwa wakurugenzi waanzilishi
wa kampuni hiyo Vicent Kigosi ‘Ray’ na Blandina Chagula ‘Johari’
kutokuwa na maelewano mazuri na sasa ikidawa kuwa chanzo ni pesa kutoka
kwa wadhamni waliokuwa  wakihitaji  kudhamini filamu inayotengenezwa na
makampuni hayo.


Chazo
hicho ambacho kipo ndani ya kampuni hiyo kilisema kuwa pesa hizo
zilitolewa na mfanyabiashara maarufu ambaye aliombwa kutoa msaada
 katika kufanikisha filamu hiyo ambayo ilikuwa iwashirikishe wasanii
kutoka Nigeria lakini imeshindikana kutokana na mgogoro wa kiuongozi
uliopo kati ya wakurugenzi hao wawili.


Chanzo
hicho kiliendelea kusema kuwa mtu wa kwanza amabaye anaonekana  sio
muaminifu katika pesa hizo ni Ray kwani mara baada ya  mfanyabiashara
huyo kukubalia pesa hizo alikuwa akienda kufuatilia msaada kinyemela
akiwa na Chuchu huku Johari akibaki ofisini.


Aliendelea
kusema kuwa Ray alikuwa akitumia mwanya wa kuwa na mahusiano na Chuchu
kwa hiyo hata walipokuwa wakitoka ofisini Johari alikuwa akijua kuwa ni
mtoko wa kimapenzi ya kawaida lakini  kumbe wao walikuwa wanakwenda kwa
mdhamini kuchota pesa za filamu hiyo.


“Baada
ya Johari kugundua kuwa kuna mchezo unaochezeka nyuma ya pazia
ndipoalipoamua kwenda moja kwa moja  kwa mfanya biashara huyo kwasababu
yeye ndiye aliekuwa connection ya  mchongo huo”.


Gazeti
la hilo liliwasiliana na Johari kwa njia ya simu kuhusiana na jambo
hilo lakina mara baada ya kupokea simu  alisema kuwa yupo kikaoni
atafutwe badae.


Kwasasa
nipo kwenye kikao siwezi kuzungumzia swa hilo nitafute badae” alisema
Johari na kukata simu.Licha ya kutafutwa badae simu yake haikuwa hewani
mpaka gazeti hilo linakwenda mitamboni. Ray hakupatikana kabisa kwenye
simu.

-udakuspecially

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.