VIJANA NA MAPENZI YAO.. UMEIPATA YA WASICHANA 17 WALIOKUTANA HOSPITALI KUMUONA BWANA MMOJA?HEBU SOMA HAPA

Admin Updates10 years ago4 Views

CB74quDWMAESkhc


Tumezoea kukutana na story za watu
kufumaniana majumbani.. kwenye nyumba za kulala wageni na kwingineko,
huyu bwana imemkuta Hospitali.. japo huwezi kuliita ni fumanizi lakini
jinsi ambavyo kagonganisha wanawake zake 17 ni ishu mtu wangu.


Yuan alipata
ajali ya gari, akawa amelazwa Hospitali March 24.. sasa kama kawaida si
kuna ndugu jamaa na marafiki wakapata taarifa kwamba ndugu yao kapata
ajali, wakawa wanakuja kumjulia hali.. mbaya zaidi ikawa pale ambapo
wasichana 17 ambao wote ana uhusiano nao walifika kwa pamoja Hospitali
tena bila kujuana.


yn

Baadhi ya wanawake na waandishi wakizungumza na Daktari.


Wang Fang ni mwanamke aliyezaa na Yuan
mtoto mmoja, amesema hakuwahi kuhisi kama mume wake ana uhusiano na
wanawake wengine, kwa sasa kajua hilo amekubali matokeo.. kasema hana
haja tena kumpenda mzazi mwenzake.


Mwanamke mwingine Xiao Li nae
alikuwa kwenye uhusiano na jamaa kwa zaidi ya miezi 18, alipata uchungu
kusikia mpenzi wake amepata ajali.. alipokutana na wasichana wengine
Hospitali wote wamekuja kumuona Yuan ilibidi uchungu wote umuishe.. ameona asahau kabisa suala la ndoa na mpenzi wake huyo.


Chinas-Romeo-Car-crash-Casanova-caught-out-at-hospital (1)

Yuan


Wanawake hao wamefungua group lao Facebook, eti kwa sasa wanajadili kuona jinsi ambavyo jamaa huyo amewachezea wote 17 kwa wakati mmoja na wasijue.
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.