Musa Mateja
Mara baada ya kuelezwa
kwamba wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi huku wenyewe wakidanganya wana
‘projekti’, hatimaye majirani wamefichua kuwa mwigizaji Shamsa Ford na
mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay’, sasa wanaishi kama mke na mume.Mwigizaji Shamsa Ford na mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay’ wakizungumza jambo.
Baada
ya kutonywa ‘mchapo’ huo, gazeti hili liliwadamkia nyumbani kwa Nay
maeneo ya Kimara-Korogwe jijini Dar na kumkuta Shamsa akiwa na kanga
moja.Mwanahabari wetu, baada ya kufika nyumbani hapo mishale ya asubuhi
alikuwa bega kwa bega kuwafuatilia ambapo alifanikiwa kugundua kwamba
wawili hao sasa wanaishi kama mume na mke.
Habari zilizopatikana
zilidai kwamba, kwa sasa Shamsa hana muda mwingi wa kukaa nyumbani kwake
kwani asilimia tisini kama si mia moja kabisa, anautumia kukaa na Nay
nyumbani hapo.Mara kadhaa mwandishi wetu amekuwa akifika nyumbani hapo
na kumkuta Shamsa akipika na kupakua huku akiwa na kanga moja huku
wenyewe wakiitana mke na mume na kuoneshana mahaba motomoto..
“Kwani
tatizo lipo wapi? Siwezi kufanya siri tena, sisi tupo kwenye uhusiano
wa kimapenzi kama unavyotuona, nimeamua kumchagua Nay kwa kuwa anajua
kupenda na kuthamini,” alisema Shamsa alipohojiwa na paparazi wetu.
Alipoulizwa Nay kulikoni ‘kumficha’ Shamsa nyumbani kwake, alifunguka:
“Yeah!
Kwa sasa hakuna project tena, hapa ni mapenzi kwa kwenda mbele, sipendi
kuwazungumzia wengine, napenda kuangalia uhusiano wangu upo vipi kwa
sasa, ninampenda Shamsa.”
Nay
na Shamsa walianza uhusiano huo mara baada ya mwanamuziki huyo kudai
kwamba alimnasa mpenzi wake, Siwema akiwa na mwanaume ndani ya sita kwa
sita hivyo kuamua kuachana naye moja kwa moja na kujikuta akiangukia kwa
mwigizaji huyo.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33





