Gladness Mallya na Hamida Hassan
MAKUBWA!
Yule bwana ambaye ni kigogo serikalini (jina tunalihifadhi kwa sasa)
aliyekuwa na uhusiano wa kimapenzi na staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu
na kumwagana naye, taarifa zimevuja kwamba kwa sasa amemnasa mwigizaji
Ester Kiama ambaye anampa jeuri ya kuishi mjini.
Kwa mujibu wa
chanzo makini, kigogo huyo ambaye anamiliki maduka kadhaa ndani ya
Mlimani City, ndiye anayempa jeuri Ester kwa kumfungulia biashara
mbalimbali na fedha kwa ajili ya kutengeneza filamu zake mwenyewe licha
ya kuwa mrembo huyo naye ana biashara zake nyingine ikiwemo ya kuuza
magari.
“Ester ana maisha mazuri mno na yote hayo anafanyiwa na
aliyekuwa bwana wa Wema, ndiyo maana unamuona sasa hivi yuko matawi ya
juu kushinda wasanii wenzake wa kike,” kilidai chanzo chetu.
Baada ya kuzipata habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Ester, mambo yalikuwa hivi:
Ester Kiama
Ijumaa: Hongera maana tunasikia sasa hivi umepata bwana mwenye nazo.
Ester: Mh! Mmeanza mambo yenu.
Ijumaa: Mambo gani wakati tumeambiwa sasa uko na yule kigogo aliyekuwa akimpa jeuri Wema?
Ester: Hahaa, nani kawaletea umbeya huo?
Ijumaa:
Sisi tunapewa habari kutoka kwa watu wanaokuona naye, wewe tuambie
umeamua kutulia hapo kwa sasa? Au huna uhusiano naye?
Ester:
Jamani haya mambo ya uhusiano ni maisha yangu binafsi, please naomba
mniache, siku zote mimi siyo mtu wa kuanika maisha yangu binafsi.”
Ijumaa: Oke tunashukuru.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33





