KUHUSU MAPENZI KATI YA WEMA NA DOGO ASLAY , HUU NDIO UKWELI ULIOPO JUU YA PENZI LAO

10 years ago118 Views


Mwanamuziki Aslay Isihaka kutoka katika kundi la Yamoto Band amefunguka
na kuweka wazi kuwa anasumbuliwa sana na watoto wa kike ndiyo maana
ameamua kuweka mahusiano yake wazi, Aslay alifunguka hayo alipokuwa akichat Live katika kipengele cha Kikaangoni Livekupitia
ukurasa wa facebook wa EATV.


Aslay alisema kuwa moja ya sababu iliyomfanya kumuweka wazi mpenzi
wake huyo ni kutaka kutoa ujumbe kwa wale ambao wanamsumbua kuwa waache
kufanya hivyo kwani tayari ana mtu ambae yeye anampenda.

“Nimeamua kuweka mahusiano yangu ya mapenzi wazi sababu nasumbuliwa
sana, nahisi kufanya hivyo wataelewa na kuacha, yaani kama
nimewapunguzia speed ya usumbufu”
Mbali na hilo Aslay aliweza kuzungumzia juu ya elimu yake na kusema
hakuacha shule kwa sababu ya muziki ila ataendelea na shule pale
alipoishia, ilaa anaamini atafanya hivyo siku za usoni.


MAHUSIANO YAKE NA WEMA


Tetesi zilizopo mtaani ni kwamba Aslay Isihaka alikuwa akifukuziwa na
Wema Sepetu kimapenzi na watu wengi walipouliza swali walitaka kufahamu
ukweli juu ya suala hilo na ndipo hapo Aslay alipofunguka na kuweka wazi
juu ya suala hilo na kusema kuwa hakuna ukweli wowote na wimbo wa
Nitakupwelepweta hajaimbiwa Wema Sepetu.


“Watu wanakuwa wanaongea mambo mengi juu ya maisha yangu hususani
katika mahusiano na kusambaza taarifa zisizo na ukweli, mfano watu
wanasema natoka kimapenzi na Wema huo siyo ukweli kabisaa bali Wema ni
kama dada yangu, ila kutokana na mambo haya ndipo niliamua kuweka
mahusiano yangu wazi ili kila mtu ajue kuwa nipo kwenye mahusiano na mtu
fulani na waache kusambaza taarifa zisizo na ukweli.”


Kwa kifupi hizo taarifa wanazosema mashabiki hazina ukweli wowote,kwa
sasa nimemtangaza mpenzi wangu na ndiye niko nae, sitaki usumbufu tena
kwa sasa.


EATV.TV

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.