TUNATOA AHADI ZINAZOPIMIKA AU ORODHA ZA MATUMAINI??…ELIMIKA HAPA KABLA YA TAREHE 25-10-2015

10 years ago97 Views

Na Mwandishi Wetu, Addis Ababa


WIKI
iliyopita nilianza kufanya uchambuzi kuhusu muelekeo wa siasa za Tanzania
kuelekea Uchaguzi Mkuu. Nilizungumzia kukosekana kwauchambuzi mujarabu kuhusu
masuala na kuahidi kuwa nitajaribu kutenga muda kuzungumzia masuala badala ya matukio
au watu.
Nilianza
kwa kujenga hoja juu ya ilani za vyama; nilieeleza historia ya ilani na kuamsha
mjadala juu ya ilani nzuri ni ipi katika kuelekea kuwapa wananchi fursa ya
kuamua kiongozi gani wamchague.
Niliahidi
kuanza uchambuzi wangu leo kwa kuiangalia ilani ya CCM kwa sababu ndiyo ilani
iliyokuwa hadharani mpaka wakati huo. Lakini kwa sababu ya matukio ya wiki hii
ambapo ilani ya Ukawa, wapinzani wakuu wa CCM, nayo imetoka, na kwa sababu ya
ufinyu wa muda, nitazijadili ilani hizi kwa pamoja, maudhui baada ya maudhui.
Katika
kujadili masuala yaliyoaihidiwa na vyama nimeona kuna vigezo vitatu vitatu
muhimu vya kupima uziri wa Ilani. Mosi ni Je, ahadi yenyewe inakidhi kiwango
cha kuwa suala linalohitaji kuwekwa katika ilani?Pili tukifungua boksi tutaona
ni mkakati gani ilani inauainisha na Je, ilani inaweka kigezo kinachopimika?

                                                               Dira ya Ilani

Tukumbushane.
Ilani sio orodha tu ya matamko na matakwa ya mgombea au Chama. Nilisema hili.
Lazima ije kutekeleza dira inayokubaliwa na wananchi wenyewe kufikia ndoto ya
Taifa.
Kwa Bahati,
kabla hatujavitumia vigezo vitatu hapo juu kwa kuziangalia sekta moja moja,
unapofanya mushabaha wa ilani dhdii ya Dira ya Taifa utabaini kuwa Ukawa haiko
wazi kuhusu uhusiano wake na Dira ya Maendeleo ya Taifa yam waka 2025 ingawa
Ilani hiyo inataja sana neno “mabadiliko.”
Katika hili
ilani ya CCM imeeleza bayana kabisa kuwa imetengenezwa kuifikia Ndoto ya
Tanzania ya kuwa nchi ya kipato cha kati kwa mujibu wa Dira ya Taifa 2025.
Hii ni
muhimu kwa sababu Ilani ikikosa kutueleza inataka kutufikisha wapi hata swali
la watatufikisha namna gani linakuwa gumu sana kuliuliza kwa sababu utafikishwaje
namna gani kama hujui unataka kufikishwa wapi?
Hii ni
kasoro kubwa katika uandishi wa Ilani za vyama vya upinzani Barani Afrika-mara
nyingi wanahemka kuandaa ilani zenye neno “mabadiliko” kuliko kuuhakikishia
umma hayo mabadiliko, kama yatafanikiwa, yanalenga kuipekleka wapi nchi na watu
wake!

Muelekeo au Mapokeo!

Kabla pia ya kuanza kuangalia ilani kwa
kina, nilitaja kuwa moja ya sifa za ilani nzuri ni lazima itupe falsafa yake ya
jumla katika muelekeo wa kuiongoza nchi. Ukizisoma ila za mataifa yaliyoendelea,
ambako nasi tunataka kufika huko, huwa zina tamko hili la muongozo wa muelekeo
wa kifalsafa.
Kwa
mfano ilani ya mwaka 1974 ya Labour ya Uingereza ilibeba anuani ya “A firm
action for a fair Britain.” Mwaka 1954 Conservatives walikuwa na ilani isemayo
kwa kifupi “The Next Five Years.”
Ilani ya
CCM katika ukurasa wa nyuma ikiashiria falsafa ya mgombea wake wa Urais ya
“HapaKaziTu” ilani inasema: “TUTATEKELEZA.” Hii inabeba ujumbe kuwa wananchi,
watendaji wa serikali na wadau wengine wa maendeleo wajiandae kwani kazi kubwa
katika miaka mitano ijayo haitakuwa maneno meeengi, bali utekelezaji!
Ni Bahati
mbaya kwamba kitabu chenye ilani ya Chadema/Ukawa hakipatikani hata kwenye
tovuti ya chama hicho lakini unaposoma hotuba mbalimbali za viongozi
wanapoifafanua ilani huoni falsafa inayohusu muelekeo wa kutekeleza Ilani zaidi
ya kauli mbinu ya mabadiliko.
                                                                
Misingi ya Ilani
Ilani pia lazima
ibebe misingi inayoweza kusaidia kufikia vision na mission ya Ilani nanchi kwa
ujumla. Ukawa wamekuja na nguzo tano ambazo ni kupunguza matumizi ya Serikali na
mashirika yake; kuimarisha utendaji na uwajibikaji; Kukuza
pato la serikali kwa kudhibiti ukwepaji na misamaha ya kodi holela, kukuza
uchumi kwa sera na sheria endelevu ikiwa ni pamoja na kukuza biashara na
uwekezaji.
Nyingine
ni kuimarisha huduma za umma kama elimu, afya, maji na makazi, na mazingira na kuimarisha
utawala bora na mfumo wa haki na sheria chini ya Katiba.
CCM
kwa upande wao wana misingi mikuu minne ya Ilani yao ambayo ni
kuondoa umaskini; kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana;
kuendeleza vita dhidi ya adui rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma; na
kuendelea kudumisha amani, ulinzi na usalama wa maisha ya wananchi na mali zao.
Katika misingi ya Ilani hizi kila Cma akimechagua kuchukua muelekeo
Fulani katika kuipa nchi maendeleo lakini Ilani ya Ukawa kukosa ahadi yoyote
katika misingi yake juu ya kupambana na rushwa na ubadhirifu ni kosa kubwa la
kiufundi.
Hii inatilia nguvu mitazamo kuwa ujio wa mgombea Urais wa Chama hicho,
Bw. Edward Lowassa unamaanisha mwisho wa upinzani kuwa na ajenda ya kupambana
na ufisadi. Katika wakati ambapo upinzani umekuwa ukijipambnanua kwa vita dhidi
ya ufisadi halafu ghafla misingi ya mapambano yake ya kutwaa dola ikakosa suala
hilo ni jambo la kustua.
Baada sasa
ya kuangalia misingi, falsafa na tangulizi kuhusu ilani hizi kuu mbili sasa
tuchambue kwa kina masuala ya msingi ambayo yamewekwa katika Ilani hizi kwa
kuangalia vile vigezo vyetu vitatu ambavyo ni:Je, ahadi husika zinakidhi
vigezo? Pili tukifungua boksi tutaona ni mkakati gani ilani inauainisha na Je,
ilani inaweka kigezo kinachopimika?

                         Elimu

Tukianza
kuchambua ahadi kwa vile vipimo vitatu nilivyovianisha hapo juu ukizisoma ni
dhahiri ilani zote mbili zimeipa elimu kipaumbele sekta ambayo huwezi kuikwepa.
Elimu ni suala muhimu nani ajenda ya wananchi katika kuona inawakomboa kutoka
walipo.
Ilani zote
zimegusia mawanda mapana ya maeneo ya kuboresha katika elimu kama vile ubora wa
elimu, kuinua elimu ya ufundi, maslahi na vitendea kazi n.k.
Ilani zote
zimeahidi elimu bure (CCM wakitaja elimumsingi yote-darasa la kwanza hadi la 12
kuwa bure, Ukawa wakitaja elimu hadi chuo kikuu kuwa bure). Swali muhimu ni Je,
kuna mkakati gani wa kutekeleza hayo na tumpime vipi mgombea ifikapo 2020?
Hakuna mkakati
kwa upande wa Ukawa wala namna wanavyoweza kupata mapato ya kutoa elimu hiyo
bure. Hii inaliacha tamko hilo zuri kubaki kuwa ahadi ya kuombea kura!
Tofauti na
Ukawa, ilani ya CCM imeainisha mikakati mbalimbali ya kutekeleza mageuzi katika
sekta ya elimu. Mfano ilani ikizungumzia ufadhili katika elimu ya juu inasema:
“Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Juu wa mwaka 2010umeandaliwa na
utekelezaji wake umechangia wanafunzi wa kidato cha sita wanaojiunga na Vyuo
Vikuu kuongezeka kutoka wanafunzi 34,564 mwaka 2009/2010 hadi wanafunzi 40,452
mwaka 2014/2015 sawa na asilimia 14.6;
Ukiacha
dosari hiyo ya ilani ya Ukawa kukosa mikakati inayoonekana, kipengele cha tatu
cha kipimo chetu pia kinaiangusha Ilani ya Ukawa; ahadi inayopimika. Waandaaji
wa Ilani ya CCM katika hili tena wameonesha ukomavu. Tazama CCM wanavyoinyumbua
ahadi ya kuboresha elimu kwa kuweka vipimo tunavyoweza kuwapima navyo (KPIs)
ifikapo 2020 wanaposema:
Mosi:
“Kuandaa mfumo, muundo na taratibu nyumbufu za kutoa Elimu ya Awali na
Elimumsingi
(1+6+4) bila malipo ili kuhakikisha kwamba:-(i) Uandikishwaji rika lengwa la
watoto wa darasa la Elimu ya Awali unaongezeka kutoka asilimia 45 mwaka 2015
hadi asilimia 100 mwaka 2020.”
Pili:
“(ii) Uandikishwaji rika lengwa la watoto wa Darasa la Kwanza unaongezeka
kutoka asilimia 95 mwaka 2015 hadi asilimia 100 mwaka 2020; na
Tatu: “(iii) Uandikishwaji rika lengwa la Wanafunzi wa Kidato cha
Kwanza unaongezeka kutoka asilimia 60 mwaka 2015 hadi asilimia 80 mwaka 2020.”
Hii maana yake ni nini? Wakati ahadi nzuri ya Ukawa ya elimu bure
tunaweza kufika hatua tukashindwa kuipima matokeo yake na kutekelezeka kwake
kwa sababu hakuna namna ya kupima, ahadi za CCM zimewekewa malengo yanayopimika
na tunayoweza kuwahukumu ifikapo 2020.
Pia katika eneo la walimu CCM inaweka ilani inayopimika na ambayo miaka
mitano ijayo tunaweza kuwahoji kwa vigezo wanaposema: “Tatizo la uhaba wa
walimu wapato 24,000 wa masomo ya sayansi na hisabati kwa shule za Sekondari
linapungua kwa kutoa mafunzo kwa walimu 5,000 wa masomo hayo kila mwaka.”
Tofauti na Ukawa wanaposema tu “tutamaliza tatizo la uhaba wa walimu.”
Labda kwa sekta hii nimalizie tu kwa kuangalia mtazamo wa Ukawa na CCM
katika kuchanghia elimu. Ukawa wanasema wao Serikali yao itatoa elimu bure
kutoka msingi mpaka chuo Kikuu.
CCM wanasema elimu msingi (msingi hadi kidato cha nne) itakuwa bure
huku vyuo vikuu ukiwepo mfumo wa mikopo. Ilani hiyo pia inaanisha wajibu wa
ushirikiano katika ya wazazi, serikali na sekta binafsi katika kuchangia elimu.
Nasema sijui, nitasubiri kuona ahadi hii ya Ukawa upepo ukiwaendea sawa
na kuunda Serikali!Lakini uzoefu wangu iwe Afrika au katika nchi zilizoendelea
Serikali haiwezi kugharamia kila kitu katika kila sekta ya umma. Haipo Serikali
ya namna hii katika dunia hii.
Uhalisia ni kwamba tamko hili ni tamu sana kulisikia lakini chungu
katika utekelezaji wake. Hii ni kwa sababu hata nchi kubwa zenye uwezo kama
Marekani haziwezi kumgharamia kila mwanafunzi elimu bure kwa kiwango cha Ilani
zetu za hapo nchini zinavyoahidi.
Ndio maana hata Marekani elimu ya juu pamoja na ufadhili mwingine,
wazazi wenye uwezo kulipia ada watoto wao Serikali pia ina Bodi ya Mikopo
iitwayo
Federal Direct Student Loan Program (FDSLP). Na pia ifahamike Bodi hiyo kwa sehemu kubwa haitoi asilimia 100
ya mikopo.

                          
Maji

Tukiachana
na sera kuhusu Elimu, maji ni eneo jingine la kiilani ambalo halipaswi
kufanyiwa mchezo. Maji ni uhai na ni muhimu kwa maendeleo na ustawi wa
mwanadamu.
Bila
kupoteza muda hapa tukiangalia ilani zinasema nini kuhusu adha ya maji?
Ukawawanasema:Tutaweka mazingira rafiki yatakayomhakikishia kwa kila
Mtanzania kupata maji safi na salama. Kumaliza kero za maji nchini kutamkomboa
mwanamke kutokana na adha ya kuchota maji kwa kichwa.”
CCM kwa
upande wao wanasema: “
Kuboresha huduma ya
maji vijijini kutoka asilimia 53.4 mwaka 2015 hadi asilimia 70 mwaka 2020 kwa
kufanya yafuatayo:- (i) Kuendelea kutekeleza lengo la kuwapatia wananchi
waishio vijijini huduma ya maji safi, salama na ya kutosha kama yalivyo Malengo
ya Milenia;
“(ii)
Kujenga vituo vya kuchotea maji 93,051 vitakavyohudumia watu 23,262,876 ambavyo
vitaongeza idadi ya watu wanaopata huduma ya maji safi na salama kutoka
20,022,283 mwaka 2015 hadi kufikia 43,285,159 mwaka 2020 sawa na asilimia 53.7;
na
Sera
inaongeza: “(b) Kuboresha huduma ya Maji Mijini kwa kufanya yafuatayo:-
(i)    Kuongeza upatikanaji wa huduma za maji katika Jiji la Dar es Salaam
kutoka asilimia 68 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 95 mwaka 2020;
“(ii)
Kuongeza upatikanaji wa huduma za maji katika miji mikuu ya mikoa kutoka
asilimia 86 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 95 mwaka 2020; (iii) Kuongeza
upatikanaji wa huduma za maji katika miji mikuu yawilaya, miji midogo na maeneo
ya miradi ya Kitaifa kutoka asilimia57 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 90
mwaka 2020;”
Ilani hizi
mbili katika eneo hili ni milima miwili rtofauti kabisa. Ukawa wanamaanisha
kuwa hawana mikakati ya utekelezaji wa wanachoahidi na watasubiri kuingia Ikulu
ndio waanze kuangalia cha kufanya. Unaposema tu “tutaweka mazingira rafiki ya
kila Mtanzania kupata maji safi na salama” kunaibua maswali.
Mosi ni
mazingira gani hayo “rafiki?” Pili yatawekwa lini na mwisho unaposema “kila
Mtanzania” tunamaanisha nini. Kwamba kufikia mwaka 2020 kila Mtanzania atakuwa
na maji safi na salama? Ni maoni yangu kuwa kwa mara nyingine tena Ukawa hawajawatendea
haki Watanzania katika eneo hili.
Wakati CCM
imekuwa wazi kama ninavyosisitiza sana humu kuhusu tunavyoweza kuwapima katika
miaka mitano ijayo, sehemu kubwa ya sera ya Ukawa, kiuhalisia, imekuwa matamko
matamu ya kuombea kura.
Tutafakari
haya kwa wiki hii na Jumapili ijayo tutachambua maeneo mengine ya kiilani kama
vile nishati, kilimo, sera za mambo ya nje na utawala bora.
Amesegnalehu
(asanteni sana).

*Mwandishi wa safu hii ni Mtanzania anayefanyakazi katika moja
ya taasisi za kimataifa jijini Addis Ababa, Ethiopia. Kitaaluma ni mtafiti
katika masuala ya siasa na maendeleo endelevu.

Endelea kutembelea Masama Blog kila uendapo kuweza kujua mambo muhimu pia yanayofanywa na Serikali na Taasisi zake katika kuletea wananchi maendeleo.
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.