MCHAMBUZI WA KIMATAIFA AFUNGUKA HOJA 10 ZA KWA NINI UKAWA WAMEIKOSA KURA YAKE 2015?..SOMA ZAIDI

10 years ago105 Views

Na Maximillan Alexander
NIMEMCHUKIA ghafla aliyekuwa Katibu
Mkuu wa Chadema, Dr. Wilbroad Slaa. Kwa aliyoyasema juzi kuhusu uchaguzi wa
mwaka 2015 nusura anipoke haki yangu ya msingi ya kujieleza kwa sababu sehemu
kubwa ya alichokijadili kimemega muktadha wa nilichokuwa nikikiandaa pia!
Hata hivyo kwa nia njema ya kuchangia
ajenda muhimu za uchaguzi zitakazotusaidia kuivusha nchi yetu hasa wakati huu
dunia inapoangalia malengo mapya ya maendeleo (SDGs 2030), nimekataa kukubali
kirahisi Dr. Slaa kunipoka haki yangu hiyo. Nitaandika machache kwa namna
yangu.
Hivyo katika makala haya, nitaeleza
kwa uchungu ni kwa nini kwa mambo haya 10 kamwe sitakuwa tayari kuiharibu kura
yangu katika uchaguzi wa mwaka huu uliopambwa na ajenda ya mabadiliko kuta
Muungano wa Ukawa na mgombea wao, Mzee Edward Lowassa.
Makala haya yatajibu swali kuu la
kitafiti la Je, hivi kuna matumaini katika safari ya Matumaini iliyoasisiwa na
Ukawa na kundi lao kwa kuuangalia Muungano wenyewe kama vyama au hata mgombea
binafsi?
1.      Mbwembwekwa malofa!
Sitaki kuharibu kura yangu kwa sababu
ya mbwembwe. Nasema hivi kwa uchungu kwa sababu nilibahatika kukutwa ghafla na
mgombea wa Ukawa, Bw. Lowassa alipotutembelea wakazi wa Mbagala. Pale alisikia
kero nyingi. Nilimshuhudia akisikiliza kwa makini. Nikajawa shauku ya kusikia
atatatua vipi kero zile kupitia ilani yake.
Siku alipokuwa Jangwani anazindua
ilani, si tu hotuba yake bali hata nilipomtazama fikra na lugha ya picha ya
mwili wake havikuonekana kama alikuwa anawakumbuka tena wale akina Mama Ntilie
wala Bodaboda wa Mbagala. Ghafla zikaja mbwembwe za Babu Seya!
Kama mpigakura hili kwangu ni doa
kubwa. Wapo watanzania wanaochanganya hili na kumuona Lowassa kama kiongozi
makini na mfuatiliaji kwa mbwembwe za kufika waliko watu maskini.Lakini juzi
nimeamini kuwa hakuwa na jingine la kutusaidia sisi malofa zaidi ya mbwembwe!
Anatuletea mbwembwe hata Malofa?
2.      Kukurupuka
Labda kutokana na taathira athari ya
hulka ya mbwembwe, kukurupuka ni sifa ya pili ya kundi la Ukawa na mgombea wao.
Kuna wakati unawaona kama watu wasiotafakari mambo kwa kina. Hivi Ukawa leo ni
watu wa kufika hatua ya kumchukua mtu kama Makongoro Mahanga-miaka mitano tu
iliyopita mlimtuhumu kuwaibia kura n ahata mkafungua kesi Mahakamani?
Labda sasa wamekutana magwiji wa sifa
hii. Vyama vinakurupuka na mgombea naye ni bingwa katika hili. Bado namkumbuka
siku Lowassa aliporejea kutoka Korea na kukukurupuka na wazo la mvua za
kutengenezwa (acid rains).
Kama si wataalamu wetu kukomaa naye
na kukataa mvua hizo zenye athari tele katika uoto wa asili Tanzania leo
ingekuwa matatani kama Taifa. Ni hatari kuihatarisha kura yangu kwa kundi hili.
3.      Vitisho
Tatizo jingine la Ukawa na wafuasi
wao ni kukosa uvumilivu wa kisiasa. Tumemsikia juzi Padre Slaa, mtu aliyetumia
muongo mmoja sasa kujitolea kukijenga Chama hicho alipokuwa na mawazo tofauti
tu vitisho alivyopokea.
Hili linanipa taswira ya Je, kura
yangu niitoe kwa watu ambao wanaweza kuja kuligeuza Taifa kuwa uwanja wa hofu
tena kwa raia wenzao wa nchi hii hii? Sio wafuasi tu hata mgombea mwenyewe Bahati
mbaya anahulka hizi.
Bado nakumbuka siku alipopewa mtihani
kidogo tu akiwa madarakani kwa mshairi mmoja kuhoji kuhusu uongozi wake katika
shairi maarufu la “Wapo Wapi Viongozi Wazuri,” Lowassa akichanganya mbwembwe, kuhamaki
na vitisho alikurupuka kujibu shairi hilo kwa shairi lake litakaloendelea
kukumbukwa kwa kukosa vina wala mizani alipodai “Tupo Tumejaa Tele.”
4.      Richmond
Katika Richmond yapo maswali mengi tu
ya kuendelea kujadili, lakini kwa sababu mdahalo umeshaombwa wa mgombea wa
Ukawa kukutana na akina Mwakyembe, mimi kama mpigakura kilio changu kikuu ni
muendelezo wa Ukawa na Lowassa kutukanganya katika suala hili.
Tuchukue mfano wa eneo moja tu-hoja
kwamba Lowassa alitaka kuvunja mkataba wa Richmond alipobaini kuwa kuna
makandokando. Juzi alisikika alipokuwa akiingia Ukawa akisema juu ya nini
kilitokea alipotaka kuuvunja.
Kwa kauli yake, alisikika akisema
kuwa alipotaka kuuvunja huo mkataba “sauti” kutoka juu iliagiza asifanye hivyo
na naye hakuhoji akakaa kimya. Hili linaibua utata juu ya ukweli na uhakika wa kauli
za Mzee Lowassa.
Nasema hivi kwa sababu akihojiwa na
Clement Mshana wa TBC (wakati huo ikiwa bado TvT) mara baada ya kuwa amejiuzulu
Uwaziri Mkuu Februari mwaka 2008, Mzee Lowassa alikuwa na hadithi tofauti
kabisa kuhusu kwa nini hasa hakuweza kuuvunja mkataba huo kama anavyodai.
Ukimsikiliza Lowasa kuanzia dakika ya
7 hadi ya 10 katika video iliyopo katika liki hii hapa chini utashangaa kusikia
mwaka 2008 akisema alizuiwa kwa ushauri wa wanasheria lakini leo 2015 anasema
alizuiwa na sauti kutoka juu! Unaweza kupoteza kura yako hapa!
5.      Kipaumbeleau kukopi mbele?
Udhaifu wa Richmond unanipa udadisi
zaidi hata wa kuangalia anayoyaahidi. Hili eneo ndio limenifanya nicheke zaidi
na kujikuta nikisisitiza tu kwamba kura yangu na yako ndugu msomaji zina
thamani sana. Amekuwa akitaja kuwa kipaumbele chake ni elimu, elimu elimu. Sina
tatizo na hilo na nafahamu huo ni mjadala wa kisomi zaidi juu ya nini kianze
kati ya vipaumbele vingi.
Tatizo langu na ambalo mwenyewe
amekiri ni kwamba ameiweka elimu kuwa kipaumbele kwa sababu alipata kumsikia
aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Toni Blair akisema hivyo! Lakini Tofauti nambwembwe
za Ukawa na Lowassa, kipaumbele cha Blair kimsingi hakikuwa elimu kwa mtazamo
wa wenzetu hawa.
Akizungumzia kipaumbele chake hiki
cha elimu katika hotuba yake aliyoitoa siku ya Jumatano Mei 23, 2001 alipokuwa
akizindua Ilani ya Elimu ya chama cha Labour mbele ya hadhira ya Chuo Kikuu cha
Southampton, Uingereza-falsafa pana ya Blair ilikuwa ni kipaumbele cha kuongeza
ubora wa huduma za umma, elimu ikiwa eneo mojawapo.
Alisema:
“If we are given a second term to serve this country, our mission will be the
renewal of our public services. There is nothing more important to making
Britain a fairer and stronger country. Our top priority was, is and always will
be education, education, education. To overcome decades of neglect and make
Britain a learning society, developing the talents and raising the ambitions of
all our young people.”
Kwa
hiyo kwanza kwa mbwembwe tu hapa muktadha wa Blair ni tofauti na Lowassa
anavyotaka tumwamini. Blair aliweka mkazo katika kufumua utendaji wa umma-elimu
ikiwa moja ya maeneo hayo.
Lakini
wakati Blair alikuwa wazi kuwa angeongeza Bajeti ya Elimu, Lowasa na Ukawa
ukienda ndani zaidi hawasemi hilo na wala kwa kiwango gani. Mbwembwe! Blair
anasema katika hotuba hiyo kwamba uwekezaji wowote katika elimu hauwezi
kufanikiwa bila kushirikisha jamii hasa wazazi, hotuba/ilani ya Lowassa hata
haikutaja neno wazazi katika sekta ya elimu. Mbwembwe tu!
Blair
yuko wazi, ameweka malengo yaliyokuwa wazi kupimika na kila mmoja. Mfano
alisema kufikia mwaka 2010 asilimia 50 ya wahitimu wote wa Sekondari wawe na
ufaulu wa kuwawezesha kujiunga na vyuo vikuu. Aliahidi kuongeza pauni 2,000 kwa
kila mshahara wa Mwalimu, Lowassa hajaweka hata lengo moja tunaloweza kumpima
nalo katika elimu. Ni matamko ya jumla tu ya kimbwembwe!
Si
lengo la makala haya kulinganisha ilani lakini walau unaona Ilani anayoinadi
Dr. Magufuli imebainisha malengo tutakayompima nayo. Kufikia mwaka 2020
Magufuli anataka tumpime kwa lengo aliloweka la kufikisha asilimia 90 ya ufaulu
wa wananfunzi wa elimumsingi. Ukiondoa mbwembwe Ukawa katika hili hawakuona
thamani ya kura yangu!
6.      Ilani
Mbwembwe za kipaumbe cha elimu
zinatuleta katika hoja pana ya ilani yao yenyewe. Mada hii peke yake inaweza
kuhitaji Makala zaidi ya nne. Lakini hapa nataka kusema jambo moja tu la kwa
nini siwezi kuwapa Ukawa na mgombea wao kura yangu. Nimesoma ilani na ahadi za
mgombea Urais wa Ukawa. Nikatabasamu kwa uchungu. Nikacheka kama mazuri vile!
Yaani hapa ni kile vijana
wanachokiita “cut and paste” tupu. Nimesoma ahadi lukuki za Ukawa na nikasoma
taarifa ya Ilani ya CCM ya utekelezaji wa miaka 10 iliyopita tu na malengo ya
miaka mitano ijayo, bila ushabiki, asilimia 95 ya Mabadiliko anayoahidi Lowassa
katika Ilani yake ama yameshatekelezwa na CCM au yatamaliziwa katika miaka
mitano ijayo!
Ngoja nitoe mifano mitatu tu kwa
sasa. Mgombea wa Ukawa anaahidi kujenga reli ya Kati!Reli hiyo tayari imo
katika Mpango wa Ukanda wa Kati na ufadhili wake uko tayari ujensi utaanza
mwaka huu baada ya diplomasia kubwa aliyoifanya Rais Jakaya Kikwete duniani
huko.
Pili mgombea wa Ukawa (tena kwa
kukumbushwa pale Jangwani) ametaja kuwa atatekeleza miradi ya maji vijijini
tena kwa sentensi tata! Katika hotuba yake amesema tu “
Kuhakikisha kuwa
wananchi wanatunza na kulinda vyanzo vya maji.” Hapa yeye kaona tatizo ni
utunzaji vyanzo vya maji, ukweli ni kwamba kasi ya utekelezaji wa sasa wa
miradi ya Programu ya Sekta ya Maji Vijijini, ilani ya Ukawa haina jipya eneo
hili.
Tatu Lowassa na
Ukawa nao wamejitutumua kuzungumzia uhusiano wa kimataifa kuwa watauboresha.
Hakuna kipya walichoonesha cha kuboresha zaidi ya matamko yale yale ya kisera
yaliyoainishwa katika Sera ya Taifa ya Mambo ya Nje-copy and paste!
7.      Waliomzunguka
Kama kuna jambo linaipa thamani kura
yangu ni pale ninapoangalia waliomzunguka au marafiki wa mgombea wa Ukawa.
Marafiki wa mgombea wanaweza kukupa visheni ya utawala wake. Sitazungumzia
makapi!
Pale alipokuwa akiongea na wahariri
mjini Dodoma kabla ya kuzindua safari yake ya matumaini mjini Dodoma, kuonekana
Lowassa bado amezungukwa na majina yenye utata kama Nazir Karamagi na wengineo ni
miongoni mwa mambo ambayo yamekuwa yakinikanganya na hata watanzania wengi
ukiwauliza watakwambia katika yote tunaweza kuelewa lakini swali litabaki kwa
nini bado yuko na hawa??!!
8.      Ukawa
Taarifa za Mzee Lowassa kujiunga na
Ukawa zimetafsiriwa kwa namna nyingi na wachambuzi. Kwangu mimi hii ni kasoro
nyingine muhimu ya kwa nini hataipata kura yangu. Sitaki kila mara kukanganywa
mimi. Leo hivi kesho vile.
Mfano, Ukawa ndio waliokuwa wakipiga
sana kelele za ufisadi na wakituaminisha kuwa Lowassa ni fisadi.Leo kajiunga
nao, ndio kusema ndimu ikiwa Tanzania ni ndimu ikiwa Ulaya ni chungwa!
Haiwezekani. Kuondoka kwake CCM na
kwenda Ukawa sit u kumegeuza geuza akili za wengi bali pia kama alivyosema Dr.
Slaa kumefifisha ajenda ya Serikali na hata ya Ukawa wenyewe katika mapambano
dhidi ya rushwa na ufuisadi kwa sababu sasa mjadala huu umepata ukakasi.
Mtuhumiwa kageuka mtumainiwa!
9.      Mabadiliko au mageresho!
Udhaifu mkubwa wa Ukawa ni kuimba
nyimbo zilizokosa maudhui. Wimbo wa Mabadiliko umekopiwa na kupestiwa kutoka
ilani na mavuguvugu ya nchi nyingi. Kwangu mimi nahitaji maendeleo zaidi,sawa,
nahitaji kuiona Tanzania yenye neema zaidi,sawa,na nahitaji mabadiliko, lakini
sioni siyaoni mabadiliko kupitia wimbo huu wa Ukawa.
Kama nilivyogusia katika udhaifu
namba 6, ilani ya Ukawa haina jipyani ukiwa mtupu. Imesheheni matamko mepesi
yasiyoweza kupimika na yaliyokosa mfumo wa kutekelezeka. Nimetaja sekta kama za
maji, sera ya mambo ya nje na reli, wamekurupuka tu kukati na kupesti!
Mabadiliko ni kufikiri, kuweka
mkakati na mfumo wa utekelezaji wenye tofauti. Kwa mfano huwezi kusema unaleta
mabadiliko kwa kuahidi kile kile ambacho CCM wameshaahidi-kujenga reli ya kati.
Kama jamaa au niseme malofa wenzetu
wa Ukawa wangekuwa wanafikiri sawasawa walau wangekuja hata na jipya la kusema
watajenga reli ya Tanga kuiinua Bandari hiyo na ukanda wa Kaskazini ili
kusafirisha hata gesi kwenda Kenya, Somalia na kwingineko!Hakuna.
Lakini kwa sababu ya mbwembwe nyingi
imekuwa ni nyimbo tu kila kukicha-mabadiliko mabadiliko mabadiliko-mabadiliko
ya aina hii yanaweza kuishia kuwa yale yale ya Iraki, Libya na Afghanistani.
Siyataki!
10.  Ubunifu
Mwisho wa siku Ubunifu (creativity)
ni moja ya sifa mujarabu za kiongozi wa karney ya 21 kwenda 22. Tunaweza
kutafsiri ubunifu kiurahisi sana-tazama udhaifu wote kuanzia namba moja hadi
tisahapo juu kiongozi/chama kikiwa na hayo makandokando yote-hakuna ubunifu ni
udunifu tu wa fikra.
Wataalamu wa masuala ya uongozi na
utawala wa jarida la Forbes katika sifa kumi za kiongozi-ubunifu ni moja uya
sifa muhimu sana. Sasa kama mtu au chama wamejaa mbwembwe-hawawezi kuwa wabunifu,
watatumia muda mwingi kufanya mbwembwe badala ya kubuni mikakati au kufanya
tafiti za kuleta maendeleo.
Jamaa
wanasema: “As a leader, its important to learn to think outside the box and to
choose which of two bad choices is the best option.” Wanasema kiongozi katika
kufanya maamuzi ya kibunifu lazima awe tayari kutoka ndani ya boksi ili aweze
hata pale ambapo uchaguzi ni kati ya mambo mawili mabaya basi walau achague baya
moja lenye unafuu.
Ndio
maana nasema wazi nataka mabadiliko lakini kwahaya ya mbwembwe, Richmond, kukurupuka
na ilani za kukopi na kupesti sioni sababu ya kupoteza thamani ya kura yangu kwa
Lowassa na Ukawa.
Mungu
akinijaalia nguvu tena nitashirikiana nayi kueleza ni kwa nini, kwa mabadiliko
wanayohubiri sasa Ukawa, nayaona zaidi katika Ilani ya CCM kuliko yao.

*Mwandishi ni mchambuzi wa masuala ya kijamii anayefanyakazi
katika taasisi ya kiraia ya Agenda2030.    

Previous Post

Next Post

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.