ABIDJAN, IVORY COAST. RAIS wa Chama cha soka cha Cameroon (Fecafoot), Samuel Eto’o ametuhumiwa kuhusika na upangaji wa matokeo na kutoa vitisho, katika faili la kustusha lililowasilishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Fifa.
Kwa mujibu wa gazeti la The Athletic, Eto’o anakabiliwa na orodha ndefu ya tuhuma zilizoelekezwa kwake zikiwamo kuhusika katika upangaji wa matokeo, kusambaza taarifa za uongo, kutoa vitisho, kusababisha vurugu na matumizi mabaya ya madaraka. Makamu wa rais wa zamani wa Fecafoot, Henry Njalla Quan Junior amelituma faili hilo kwa Fifa na pia linachunguzwa na Caf. Shirikisho hilo la soka la Afrika pia limethibitisha kuwa linachunguza kuhusiana na madai hayo dhidi ya Eto’o na Fifa iliwahi kushauriwa kumtoa staa huyo wa zamani wa Barcelona katika nafasi yake kutokana na mfululizo wa matukio tata.
KUPANGA MATOKEO
Njalla Quan Junior amedai kwamba mechi kati ya akademi yake na Kumba City FC ilipangwa matokeo na Eto’o, akieleza tukio hilo kama moja ya “kashfa kubwa kabisa maishani”.
Bosi huyo wa Cameroon pia anatuhumiwa kupanga matokeo ya timu ya “rafiki yake wa karibu“ Valentine Nkwain ipande daraja. Victoria United ikapanda daraja baada ya kushinda mechi 11 kati ya 17 za mwisho wa msimu licha ya kupoteza mechi nne kati ya saba za kwanza za msimu huo.
Gazeti la The Athletic likaongeza kuwa uhusiano wa Njalla Quan Junior na Eto’o uliharibika kabisa, na ukasababisha straika huyo wa zamani kudaiwa kumlipa mtu atume meseji ya vitisho. Ilisomeka: “Mimi ni mafia wa mapinduzi haya na katika umafia huu hatuwasaliti viongozi wetu. Nimekuwa nikilinda maslahi ya mipango yetu hadi leo. Hivyo, kama utanizingua kaa tayari kubeba mzigo wa kitakachotokea.”
UNAIKUMBUKA HII?
Eto’o alirekodiwa video akimkandamiza kwa goti usoni mtu baada ya mechi ya Brazil dhidi ya Korea Kusini katika fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar. Gwiji huyo wa Cameroon alikuwa akihudhuria mara kwa mara mechi za nchini Qatar.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







