
Kama inavyoeleweka kuwa game ya music kwasasa ime-change tena kwa kiasi kikubwa sana, kiasi kwamba baadhi ya vitu vilivyo kiki zamani kushindwa kuchukua nafasi kwasasa.
Tume washuhudia mastaa kibao ambao waliumiza kinoma noma hapo awali lakini hali imekuwa ngumu kwa wao kurudi kwenye mstari kwasasa, kutokana na hali ya muziki jinsi ilivyo, muziki ambao unahitajika kwenye soko la sasa na vitu kama hivyo.
Moja kati ya vitu ambavyo vilikuwa vina-shine kinoma noma kipindi cha nyuma ni muziki wa makundi. Ikiwa tuliyashuhudia makundi kibao kama East Coast, TMK Wanaume Family na mengineyo kibao yakifanya vizuri sana katika game na kuleta ushindani wa hali ya juu.
Lakini hali imebadilika kwa kiasi kikubwa sana siku hizi na kupelekea makundi kupotea kabisa katika ramani ya music. japo kuwa yapo machache ambayo bado yenaendelea kufanya lakini sio kwa nguvu ile kama ilivyokuwa hapo awali.
Perfect255 imepiga story na Mwana FA ikiwa ni mmoja wa wasanii ambao walikuwa chini ya kundi la East Coast na kutaka kujua mipango yake katika kurudi kufanya muziki wa kundi kwa soko la sasa, na alikuwa na haya ya kusema.
“Nafkiri tunaweza kufanya kazi kwa pamoja, yaani watu wawili, watatu hadi wanne lakini kutengeneza group as a group kwa uchumi wa kimuziki ulivyo sasa hivi itakuwa ni kazi kubwa kidogo. Tunaweza kufanya group ya project, kama tunataka kufanya project hii tukaifanya mwanzo hadi mwisho ikimalizika kila mtu akashika hamsini zake, lakini hakuna uwezekano wa kutengeneza group na ikafanya kazi kama group moja kwa moja, muziki wa group ulisha shindwa.”
Play hii video hapa chini kumsikiliza Mwana FA akifunguka mwanzo hadi mwisho na kiufafanuzi zaidi kuhusiana na suala hilo.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






