ANC WAONGOZA UCHAGUZI WA AFRIKA KUSINI

7 years ago128 Views

CHAMA tawala cha Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ANC kitahifadhi wingi wake wa viti bungeni baada ya uchaguzi, ijapokuwa umaarufu wake utapungua na hivyo kuathiri jitihada za kukifufua chama hicho na pamoja na uchumi unaoyumba wa nchi hiyo. 

African National Congress, ambacho kimekuwa madarakani tangu 1994, kinaendelea kuongoza kikiwa na karibu asilimia 57 ya kura baada ya zaidi ya nusu ya maeneo ya kupigia kura kuhesabiwa rasmi kutokana na uchaguzi uliofanyika Jumatano. 

Ramaphosa mwenye umri wa miaka 66, alichukua usukani mwaka jana baada ya chama hicho kumlazimu aliyekuwa rais wakati huo Jacob Zuma kujiuzulu baada ya miaka tisa iliyozongwa na madai ya rushwa na matatizo ya kiuchumi. Matokeo yaliyotolewa na tume ya uchaguzi yanaonyesha kuwa mpinzani wa karibu kabisa wa ANC, chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance – DA kinafuata na asilimia 23. 

Wakati Chama cha Economic Freedom Fighters kikiongozwa na Julius Malema ni cha tatu na asilimia 10. Matokeo rasmi yanatarajiwa kutolewa kesho Jumamosi ya Mei 11,2019. 

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2E1n3Fp
via

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.