Ikulu, Dar es Salaam
Rais Dk. John Magufuli amemteua Rais mstaafu Benjamin Mkapa (pichani), kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ikiwa ni kipindi cha pili mfululizo.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu jijini Dar es Salaam, imesema pi Rais Dk. Magufuli amemteua Prof. Ignas Rubaratuka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA). Prof. Rubaratuka ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa kipindi cha pili mfululizo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi wa viongozi hao umeanza tangu tarehe 10 Mei, 2019
from CCM Blog http://bit.ly/2HiFhEC
via

