HANSCANA AWATOLEA POVU VIJANA VIZUIZI WA MAENDELEO KWA WENZAO.
Na.Khadija Seif, Michuzi TV
Muandaaji na mtayarishaji maarufu wa video za muziki nchini Hance Richard (pichani) maarufu kama Hanscana amepasua jipu kwa watu wote wanaoweka vikwazo katika mafanikio na ndoto za wenzao.
Hanscana kwa sasa anamiliki moja ya kampuni kubwa sana ya utayarishaji wa video za muziki ijulikanayo kwa jina la Hanscana brand ambapo ameajiri waaongozaji wengi vijana ili kufanya kazi pamoja na kuwaachia ujuzi tofauti tofauti.
Hanscana ambaye anaendelea kufanya vizuri kwenye tasnia ya utayarishaji wa video za muziki na kuleta mapinduzi makubwa na kufanya kazi nyingi sana zenye ubora sawa na za watayarishaji wakubwa kama Justin Campos kutoka afrika kusini ,Mr.moe musa kutoka nchini nigeria.
Tasnia hiyo kwa kiasi kikubwa itaendelea kukua siku hadi siku kutokana na ubora wa video hizo kama cheche ya ommy dimpoz, subalkheri ya aslay, wasikudanganye ya nandy, utaniua ya jux na zingine nyingi za wasanii mbalimbali.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameandika kuwa “Ukishindwa kuwa daraja kwa wenzio basi usiwe ukuta”, akimaamisha kuwa vijana wanatakiwa kuthamini na kupongeza juhudi za mtu mwingine pasi na kuwa kizuizi wa juhudi hizo au kubeza.
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2VGnxvy
via

