Wananchi na walipa kodi Mkoani Kagera wametakiwa kuzingatia Elimu ya kodi waliyoipata katika wiki ya Elimu kwa mlipa kodi, na kuwa tayari kupokea mabadiliko mbalimbali ya kodi na usimamizi wake Kwa masilahi ya Taifa.
Wito huo umetolewa Wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Elimu kwa Mlipa Kodi, ambapo Mkoani Kagera yamefanyika katika Uwanja wa Uhuru Manispaa ya Bukoba, Mei, 17 yakihudhuriwa na wananchi, wafanyabiashara, wanafunzi na wadau mbalimbali.
Katika hotuba ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Kagera, iliyosomwa kwa niaba yake na Mwakilishi katika maadhimisho hayo Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Ndg. Projestus Rubanzibwa ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Kagera kuendelea kutoa Elimu na Hamasa kwa Umma ili walipa kodi waendelea kulipia kodi zao sahihi na Kwa wakati, bila shurti, kutoa Elimu ya Ufahamu ya mabadiliko mbalimbali ulipaji kodi kupitia simu, matumizi ya mashine za Efds hii itachangia kwa mlipa kodi kwa mzalendo na kutimiza wajibu wake kwa maendeleo ya Taifa.
Awali akitoa salaam zake kwa niaba ya Meneja Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mkoani Kagera, amesema changamoto kubwa miongoni mwazo ni pamoja na mwitikio mdogo wa wafanyabiashara katika Elimu ya ulipaji kodi, matumizi kidogo ya EFDs, wananchi kutoomba lisiti wanaponunua bidhaa.
Maadhimisho hayo yaliyoanza Mei 13, 2019 yenye kauli mbiu ya “Karibu Tukuhudumie” yameambatana na usikilizwaji wa kero, ushauri na maoni kutoka kwa wananchi na walipa kodi, huku yakipambwa na burudani safi kutoka kikundi cha KAKAU BAND.
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2Vzv6zv
via







