Wakili wa serikali Candid Nasua amewataja washtakiwa hao kuwa ni, Godlisten Mtui, mfanyabiashara, Frank Lucas dereva wa pikipiki na Mhando Shomary, Mkulima
Mbele ya Hakimu Mkazi Maila Kasonde imedaiwa, Mei 7 mwaka huu, huko katika eneo la Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, washtakiwa, walikutwa na vipande vinne vya meno ya tembo vya USD 30000 ambazo ni sawa na Sh. 69,025,000 bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.
Aidha washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka la utakatishaji, ambapo wanadaiwa kumiliki vipande hivyo vya meno ya tembo huku wakijua wakielewa fika kuwa, vipande vivyo vya meno ya tembo vimetokana na kosa la uwindaji haramu.
Hata hivyo, washitakiwa hao hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kw kuwa, mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hadi Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP), atakavyoelekeza vinginevyo.
Washitakiwa wote wamerudishwa rumande hadi Juni 4 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2YyBKb0
via

