I love you so much!Hivyo Sheikh Hilaly Makakara maarufu Sheikh Kipozeo alivyomwambia Rais Dk.Joh Magufuli baada ya kukutana naye jijini Dar es Salaam wakati wa Shirika la Simu Tanzania(TTCL) likikabidhi gawio kwa Serikali.
Sheikh Kipozeo amepata nafasi hiyo leo Mei 21,2019 wakati alipopata nafasi ya kuomba dua kabla ya kuanza kwa tukio la utoaji gawio kwa Serikali kutoka Shirika la Simu Tanzania(TTCL) ambapo Rais Magufuli alikuwa mgeni rasmi.
Wakati anaitwa kusoma dua ,Mshereheshaji wa tukio hilo Tom Mushi ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TTCL amesema Sheikh huyo amekuwa akitamani kumuona Rais Magufuli kwa karibu.
Mushi alisema ” Sheikh Kipozeo amekiwa akionekana mitandaoni mara kwa mara akisema anatamani siku moja aonane na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli kwani kuna jambo anataka kumueleza.Sheikh Kipozeo karibu umwambie Rais unachotaka kumwambia.”,
Baada ya ukaribisho huo Sheikh Kipozeo alianza kwa kuomba dua na kisha akamwambia Rais Magufuli kwamba “I love you. Mimi ni sheikh wa Rufiji huko, na Rais wangu anatoka Mwanza.Narudia tene I love you,” amesema Sheikh huyo mbele ya Rais.
Amesema anayo sababu kubwa ya kumpenda Rais Magufuli na mojawapo ni namna ambavyo Rais amekuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo kwa ajili ya nchi yetu akitolea mfano ununuzi wa ndege nane.
“Hatukuwa na ndege hata moja lakini Rais Magufuli amenunua ndege nane na binafsi nimezionja ,nimepanda kwenda Mwanza na kurudi na nimepanda kwenda Burundi.Tunakushukuru Rais kwa namna ambavyo unaitumikia nchi yetu kwa uzalendo mkubwa.
” Kazi yetu ni kuhakikisha tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu ili uwe na afya njema kuendelea kulitumia taifa letu la Tanzania,”amesema Sheikh Kipozeo na kusisitiza amefurahi sana kumuona Rais Magufuli kwa karibu zaidi kwani ilikuwa ndoto yake ya siku nyingi.
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2HsUy5M
via

