
Takwimu hizo zimetolewa katika kikao kilichokutanisha wadau mbalimbali mjini Nzega na shirika lisilo la Kiserikali la World Vision linaloendesha kampeni hii ya kupambana na Mimba na ndoa za utotoni likishirikiana na Serikali ili kutokomeza janga hili ambalo linakwamisha ndoto za Watoto wa kike
Bertha Mtesigwa ambaye ni Mratibu wa shirika la world Vision amesema Mradi huo una miaka saba ukitekelezwa na shirika hilo Lakini tatizo hilo linendelea kupungua japo amesema chngamoto haziishi
“Mimba hizi zimechangiwa na Sababu mbalimbali ikiwemo ya kwanza ni umasikini uliokithiri kutoka katika jamii zetu za watu wa Nzega Lakini kumekuwa na uelewa mdogo kuhusu suala la Malezi Makuzi ya mtoto na mila potofu ambazo zimechangia sana kuongezeka kwa mimba za utotoni “Amesema Mtesigwa
Meneja wa shirika la world Vision John Masenza amesema vyombo vya dola vinaendelea kupambana na tatizo hilo na amewaomba Wananchi Kushirikiana na shirika hilo ili kukomesha mimba za utotoni
Aidha idadi kubwa ya wanaopata mimba za utotoni ni wanafunzi wa shule za Msingi na shule za Sekondari.
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2Ke7MoG
via






