MKURUGENZI wa bendi ya taarab first classic modern, Abubakari soud (Prince Amigo) amesema muziki wa taarab hautokufa na utaendelea kuwepo.
Amigo amesema kuwa muziki wa taarab ulianza zamani na utaendelea kuwepo kutokana na uwepo wa mashabiki na wadau wa muziki huo wa mwambao.
“Waliopotea ni baadhi ya mashabiki na sio muziki wa taarab kwani waimbaji wakali bado wapona wanaendelea kuongezeka kila siku.” ameeleza Amigo.
Aidha, ameeleza kuwa utofauti wake kwa sasa kuwa yupo kwenye utawala mpya ambao anafanya kazi akiwa Kama mkurugenzi na mmiliki wa bendi hiyo ya first classic modern taarab.
“Nilikua jahazi na nililelewa vizuri ili niweze kukua kimuziki na ndio sababu kubwa imefanya nimeweza kuwa na uthubutu na kusimama imara na bendi yangu.” Ameeleza.
Pia ameeleza kuwa tabia ya baadhi ya waimbaji wakike kuponda uongozi walipotoka pindi wanapoahamia kwenye uongozi mpya kuwa si jambo zuri kwani inajenga uhasama baina ya muimbaji na uongozi wa awali ama kati ya bendi na bendi.
“Waimbaji wakike ndio wanaongoza kwa tabia hiyo hivyo wajifunze kuheshimu uongozi walipotoka kwani binafsi nimefanya kazi bendi tofauti kama east Africa melody na jahazi hata baada ya kuondoka sikuwahi kuongea vibaya japo wote ni binadamu hakuna mkamilifu kuna matatizo mawili matatu” ameeleza Amigo.
Pia amesema kwa sasa anategemea kuzindua albamu yake mpya “mama wa hiyari” aliyomshirikisha malkia wa mipasho khadija kopa.
Vilevile ametoa rai kwa wamiliki wa bendi za taarab kuwapa faraja wasanii wao na kushirikiana nao kwa hali na mali. “Kuwepo kwa mahusiano mazuri kati ya viongozi hadi kwa waimbaji ndipo kazi itafanyika kwa ufanisi na kuepusha minong’ono isio na tija” ameeleza.
from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2KhFtGV
via

