Mantrac ndio waliopewa idhini ya kushughulikia bidhaa za Caterpillar nchini Tanzania, wakisambaza na kuhudumu katika mashine za CAT.
Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Meneja Mauzo wa Mantrac Tanzania, Butwa Sanga, alisema kwamba katika kujaribu kwenda kwa hali ya juu na kasi ya viwanda, kampuni hiyo inayoshughulikia mashine zenye uwezo mkubwa imekuja na chapa mpya ya Caterpillar yenye ufanisi mkubwa na inayookoa muda.
Alitambulisha mashine mpya kuwa ni New Generation Hydraulic Excavator (NGH) Caterpillar itakayoleta mapinduzi makubwa kwenye ajenda ya kuelekea kwenye nchi ya viwanda, kwa sababu ina ufanisi wa hali ya juu, gharama ndogo na inachukua muda mfupi kukamilisha kazi.
“Viwanda havijengwi kwa mkono, vinahitaji mashine zenye uwezo mkubwa kufanya hivyo, na kwa kutumia mashine hizi mpya za NGH Caterpillar zilizoingia sokoni, tunatarajia kwamba watu waliojipanga kujenga viwanda vipya watapata kile kinachofaa sana kwa kazi hiyo ili kwenda haraka, tofauti na modeli zile za zamani,” alisema.
Bw. Sanga alikuwa akizungumza kwenye mafunzo ya siku tatu yanayokwenda kwa jina la ‘Changamoto ya Mafundi’ ambapo Mantrac inatoa mafunzo kwa mafundi 30 juu ya jinsi ya jinsi ya kutumia caterpillars hizo mpya zenye teknolojia ya hali ya juu.
Alisema kwamba makatapila hayo mapya ya NHG yanapunguza muda wa kazi kwa nusu na wakati huo huo kupunguza matumizi ya mafuta kwa kati ya asilimia 25 na 45 huku yakiongeza tija na uzalishaji.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2XxmIFp
via


