Baada ya kutembelea mabanda hayo, Pinda amesema hawezi kufananisha Maonesho hayo na mengine mengi yaliopita kwani amebaini mengi katika maonyesho haya ikiwemo wafanyabiashara walioshiriki wamekua kibiashara, vifungashio vimeboreshwa, bidhaa na pia kuna mpangilio mzuri wa vitu.
Aidha amezisisitiza Mamlaka husika zinazosimamia na kudhibiti bidhaa na vyakula ikiwemo Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Shirika la Viwango Nchini (TBS) kutokubweteka badala yake ziendelee kusimamia zaidi ili waweze kushindana kimataifa.
“Biashara katika Maonesho haya zimeboreshwa lakini pamoja na mafanikio haya Mamlaka zinazohusika na Udhibiti zisibweteke zikazane kusimamia zaidi ili tuweze kufika katika soko la ushindani la kimataifa”alisema Pinda
Ameongeza kuwa, kati ya vitu vingine alivyovibaini katika Maonesho haya kuwepo kwa mwitikio mkubwa wa bidhaa za asali .
Pinda amesema katika Maonesho yaliyopita Asali ilikuwa miongoni mwa bidhaa ambazo zilikuwa adimu lakini sasa nimefurahi kuona zao la Asali limeonekana kuwa maarufu katika maonesho haya,nimekutana na watu wengi wanaouza zao hili.tuomba watu wajiwekeze zaidi.
Aidha ametoa wito kwa Wananchi ambao awajafika katika Maonesho haya kujitokeza kwa wingi kuja kuona Mambo mbalimbali ikiwemo vilivyomo
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2xywcSs
via

