Mkurugezi na Mmiliki wa kampuni ya Bakhresa Group of Companies Said Salim Bakhresa(kushoto) akizungumza na Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe(katikati) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati wa kugwa kwa miili ya wafanyakazi watano wa Azam waliofariki kwenye ajali walipokuwa njiani kwenda kurusha matangazo mbashara ya uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato.
Wafanyakazi wa Azam TV waliofariki kwenye ajali hiyo ni Salim Mhando (muongozaji wa matangazo), Florence Ndibalema (Mhandisi wa Sauti), Sylvanus Kasongo (Mhandisi Mitambo) na wapiga picha wawili Said Haji na Charles Wandwi.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/30qWpi9
via








