Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV – Kagera.
Serikali ya Mkoa wa Kagera imeendelea kutekeleza kwa vitendo ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015 – 2020 kwa kuhakikisha wakazi wa Mkoani Kagera wanaondokana na hali duni kwa maendeleo endelevu.
Akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi, mbele ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti, amesema kuwa Mkoa wa Kagera kwa ujumla umeendelea kuhakikisha unajikwamua kiuchumi kwa kuweka miundo mbinu sahihi katika kila sekta, ili kufanya mazingira rafiki kwa mwananchi katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku.
Mhe. Gaguti amesema pato la Mkoa limeongezeka kupitia makusanyo ya Halmashauri za Wilaya na kufanya mapato ya Mkoa kufikia shilingi Bilioni 48.747 kwa mwaka 2018/19 ukilinganisha na makusanyo ya shilingi Bilioni 44.162 kwa mwaka wa fedha 2017/18.
Aidha katika sekta za Afya, Uvuvi, Kilimo, Elimu Mkoa umendelea kutekeleza Ilani kwa kuweka mazingira bora kwa kuendeleza ujenzi wa zahanati, vituo vya Afya na Hospitali tatu mpya za Wilaya, sambamba na ujenzi wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu maabara na Vyuo vya Ufundi VETA.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera Bi. Costancia Buhiye akisisitiza jambo mara baada ya Kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015-20 kwa Mkoa wa Kagera.
Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Mhe. Gaguti wakati akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani katika ukumbi waHalmashauri ya Bukoba.
Pichani ni Mbunge wa Viti maalum Kagera anaewakilisha Vijana Mhe. Halima Bulembo akichangia taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM Mkoa wa Kagera, kubwa akisisitiza ujenzi wa kituo kikubwa cha Uwekezaji Mkoa wa Kagera.
Pichani Mweyekiti wa CCM (W), Bukoba Ndg. Joas Muganyizi Zachwa akitoa shukrani zake kwa Utekelezaji wa Ilani zaidi akiomba marekebisho upande wa sekta ya Afya.
Pichani ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera wakiendelea kufuatilia mkutano wa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa Ilani 2015-20
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2YmF3FO
via





