Jamii imeshauriwa kuwa na moyo wa upendo na kujitolea katika kuwasaidia watu wenye ulemavu ambao wengi wao wanaishi katika dimbwi kubwa la umasikini.
Hayo yamesemwa na Bi Theresia Kazimoto mkazi wa Kata ya Laroi mwenye watoto wanne ambao wote wanaulemavu.
Bi Theresia ameyasema hayo alipotembelewa na mbunge wa Viti Maalum Amina Mollel aliyeitembelea familia hiyo nyumbani kwao Laroi na kujionea mateso anayopata mwanamke Huyo katika kuwalea watoto hao.
Akiwa nyumbani hapo, Mbunge huyo ameisaidia familia hiyo mahitaji mbalimbali na kuahidi kurudi tena ili kufuatilia majibu ya vipimo vilivyopelekwa katika hospitali ya KCMC.
Mbunge wa Viti Maalum,Amina Mollel akifurahia jambo na Watoto wane wenye ulemavu .
Mbunge wa Viti Maalum,Amina Mollel akiwa katika picha ya pamoja na watoto wane wenye ulemavu sambamba na Mzazi wao pamoja na wasaidizi wa Mbunge huyo.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2YaeSCO
via


