Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango awataka Waajira wapya wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma.
Hayo ameyasema alipofanya nao kikao cha kuwakaribisha wizarani hapo Jijini Dodoma, ambacho kilihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Utawala Dkt. Khatibu Kazungu, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Sera Bw. Adolf Ndunguru na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara hiyo.
Akizungumza katika kikao hicho Dkt. Mpango alisema kuwa anatarajia kuona watumishi hao wanafanya kazi kwa kwa bidi na kujituma, na kuwa wazalendo kwa nchi yao.
“Umasikini wa watanzania uwasukume kufanya kazi kwa bidii, nchi ina rasilimali nyingi lakini asilimia 26.4 ya wananchi bado hawapati mahitaji ya msingi hivyo tufanye kazi kwa bidii kusaidia watu kuondokana na umasikini.”Alisisitiza Waziri Mpango.
Aliwataka Watumishi hao kutumia ujuzi wao kufanya kazi kwa weledi mkubwa kwa hadhi ya kimataifa kwa kuzingatia uadilifu na uaminifu katika kutekeleza majukumu yao.
AIDHA, Dkt. Mpango amewataka Viongozi wa Wizara hiyo, kuwapa ushirikiano Watumishi hao na kuwa tayari kuwasaidia na kuwaelekeza katika majukumu yao watakayo wapangia lakini pia wawe tayari kujifunza kutoka kwao.
‘’Muwe tayari kuwasikiliza na kuwasaidia watakapopata changamoto katika utekelezaji wa majukumu yao”,alisema Dkt. Mpango.
Aliwataka Watumishi hao kuhakikisha wanajiendeleza kielemu wanapopata nafasi na kutoridhika kwa elimu waliyokuwa nayo kutokana na ukuaji wa teknolojia.
Dkt. Mpango alisema Wizara hiyo inamajukumu mengi takribani 20 ikiwemo kubuni na kusimamia sera za bajeti, fedha,ununuzi wa umma pamoja na ubia kati ya sekta za umma na sekta binafsi.
Aliongeza kuwa utekelezaji wa dira ya Taifa, kupanga na kutekeleza mandeleo ya uchumi yaende wapi, pia ina jukumu la kuandaa muongozo wa bajeti ya Serikali na utekelezaji wake.
Naye mmoja wa Waajiriwa wapya ameishukuru Serikali kwa kutoa ajira na kuahidi kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia madili ya Utumishi wa Umma.
Jumla ya Watumishi wapya 70 wa kada mbalimbali wakiwemo Wachumi na Wasimamizi wa Fedha wameajiriwa katika Wizara ya Fedha na Mipango ikiwa ni ajira yao mpya.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasimali Watu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Michael John akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Adolf Ndunguru aweze kumkaribisha Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Philip Isdor Mpango ili aweze kuzungumza na Waajiriwa wapya wa Wizara hiyo (hawapo pichani), Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Adolf Ndunguru akimkaribisha Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Philip Isdor Mpango aweze kuzungumza na Waajiriwa wapya wa Wizarahiyo mkoani Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Waajiriwa wapya, alipofanya nao mkutano Jijini Dodoma na kuwataka waajiriwa hao kufuata maadili ya Utumishi wa Umma.
Baadhi ya Waajiriwa wapya wa Wizara ya Fedha na Mipango wakimsikiliza Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Philip Isdor Mpango (hayupo pichani), alipokuwa akizungumza wakati wa kikao Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo vya Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia kwa karibu kikao cha Waajiriwa wapya wa Wizara hiyo, kiliongozwa na Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Philip Isdor Mpango (hayupo pichani), Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Waajiriwa wapya, alipofanya nao mkutano Jijini Dodoma.
Meza kuu ikiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulika Utawala Dkt. Khatibu Kazungu, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia Sera Bw. Adolf Ndunguru na Mkurugenzi wa Utawala na Rasimali Watu wa Wizara hiyo Bw. Michael John wakiteta jambo wakati wa kikao na Waajiriwa wapya (hawapo pichani) Jijini Dodoma.
Mwajiriwa mpya akitoa neno la shukrani kwaniaba ya Waajiriwa wapya kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango kwa kutenga muda wake na kuzungumza nao Jijini Dodoma, na kuahidi kutekeleza kwa ufanisi majukumu watakayopangiwa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulika Utawala Dkt. Khatibu Kazungu akimshukuru Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Philip Isdor Mpango (hayupo pichani), kwa kutenga muda wake kuzungumza na Waajiriwa wapya wa Wizara hiyo Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulika Utawala Dkt. Khatibu Kazungu, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia Sera Bw. Adolf Ndunguru na Mkurugenzi wa Utawala na Rasimali Watu wa Wizara hiyo Bw. Michael John na Katibu wa TUGHE Bi. Jenjelly James wakiwa katika picha ya pamoja na Waajiriwa wapya baada ya kumalizika kwa kikao Jijini Dodoma.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Ygf5EK
via










