Na Editha Karlo wa michuzi tv Kigoma .
Msanii wa Bongo Fleva na Diwani wa kata ya Mwanga kaskazini kupitia cha cha ACT Wazalendo katika Manispaa ya Kigoma Ujiji,Revocatus Kipando maarufu kama Baba Levo amehukumiwa leo kifungo cha miezi mitano kwa kosa la kumshambulia Askari wa Usalama Barabarani wakati akitimiza majukumu yake ya kazi.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Frolence Ikorongo wa mahakama ya Mwanzo mwandiga alisema mshtakiwa amekutwa na kosa katika kesi iliyo kuwa inamkabili hivyo mahakama inampa adhabu ya kutumikia kifungo cha miezi mitano jela. Baba Levo alikuwa na kesi ya kumshambulia askari wa barabarani wakati akiwa kwenye majukumu yake ya kazi.
Tukio la kumshambulia askari lilitokea July 15 majira ya saa moja usiku katika eneo la kwabela ambapo baba Levo alimshambulia askari wa barabarani anayefahamika kwa jina la Msafiri Ponera wakati akiwa kwenye eneo lake la kazi.
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa alilazimisha kupita kwa pikipiki eneo la watembea kwa miguu wakati askari huyo ameshawaruhusu watembea kwa miguu kuvuka,baada ya hapo baba levo alimua kumshambulia askari huyo. Diwani wa kata ya Kigoma mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo Hussein Kaliyango amesema kuwa tayari wameshaanza mchakato wa kukata rufaa ili haki ya baba Levo ipatikane.
“Tunashukuru maamuzi ya mahakama tunakata rufaa leo hii tunaingiza rufaa tunaamini haki ya Baba levo itapatikana, Niwatoe hofu wananchi wa kata ya mwanga kaskazini kuwa tunakata rufaa tunaimani mahakama itatenda haki”alisema Diwani huyo Alisema Baba levo ni mtetezi wa Bodaboda,Bajaji na wanyonge wajasiliamali katika Manispaa ya Kigoma amewapambania vya kutosha leo amepatikana na hatia kwa nia ya kuwatetea wananchi wa mji mzima ndio alivyozaliwa baba levo hii ndio safari ya kuwa mwanasiasa mkubwa nchini.
Msanii wa Bongo Fleva na Diwani wa kata ya mwanga kaskazini kupitia chama cha ACT Wazalendo Revocatus Kipando maarufu Baba Levo akitoka mahakama ya mwanzo ya Mwandiga baada ya kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela kwa kosa la kumshambulia askari wa usalama barabarani akiwa kazini.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2KbxkCG
via

