Mbunge huyo wa Temeke ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema hayo jana katika kongamano lililoandaliwa kwa mara ya kwanza na Taasisi Open Mind ambayo iko chini ya Mwenyekiti Abel Otieno ambaye pia ni maarufu kwa jina la ‘MC Rhevan’,lililowakutanisha vijana na wasajasiriamali lililofanyika katika hoteli ya Lamada Jijini Dar es Salaam.
Aidha Mtolea amesema kuwa vijana wengi wamekua hawana elimu ya kujitegemea hasa katika kujiajiri na kujiwekea malengo ya kuweza kupata ajira binafsi huku akiwataka vijana kuangalia nchi inakwenda kwapi ili wasiweze kuachwa njiani huku akiwataka vijana wajifunze kutenda mambo kwa viyendo kuliko kuwa wazungumzaji zaidi ili mwisho wa siku jamii iweze kuyaona matunda ambayo yamezalishwa na vijana wake.

“Usipojitumia kama wewe mwenyewe kijana basi wenzako waliokuzunguka watakutumia sisi wanasiasa tutakutumia na watu wengine watakutumia sababu watu wengi wanapenda kuwatumia vijana kwakuwa ndiyo kundi kubwa ambalo mtu akilitumia ataweza kufanikisha jambo lake hivyo tambueni kuwa mwisho wa siku unayoyafanya leo ndiyo utakayovuna kesho”alisema Mtolea.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2KIlVsT
via



