Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete amesema waandaji wa mbio za nyika za Brazuka kwa ajili ya kuchangia watoto wanye matatizo ya moyo, wamefanya jambo jema katika kuokoa maisha ya watoto zaidi ya 500.
Dkt Kikwete katika mbio hizo alishiriki kwa kutembea Kilomita Tano (5KM) ikiwa ni kuimarisha afya pamoja na kuunga mkono marathon hizo za kuchangia watoto hao.
Akizungumza baada ya kumalizika mbio hizo, Dkt. Kikwete amesema kuwa licha ya kuchangia watoto hao kwa walioshiriki kwa mwitikio mkubwa wameimarisha afya kwa kutoa sumu mwilini.
Amesema kuwa kwa waandaji Brazuka waendelee kuandaa marathon hizo kwa kila mwaka kutokana na kuwepo kwa mwitikio wa jamii katika uchangiaji fedha zitakazosaidia watoto wenye matatizo ya moyo na kuokoa maisha yao.
Aidha amesema kuwa benki 18 zilizoshiriki katika marathon hizo wamejitoa katika kufanikisha marathon hizo kwa wao wenyewe kukimbia.
Dkt. Jakaya Kikwete amewashukuru wadhamini kwa kutoa mchango yao katika kufanikisha mbio hizo za marathon.
Naye Mratibu wa Marathom hizo za Brazuka, Nasikiwa Berya amesema kuwa ni mara ya kwanza kuandaa mbio za nyika hivyo wataboresha changamoto zilizojitokeza katika marathon hizo.
Amesema kuwa mwitikio wa marathon hizo umekuwa mkubwa na kufanya kumtia moyo wa kuendelea kuzifanya ikiwa ni kupokea maagizo ya Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete ya kufanya kila mwaka.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi amesema kuwa marathon kwa ajili ya watoto wenye matatizo ya moyo ni jambo muhimu ili kuweza kuwatibia katika taasisi hiyo.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/300jT1F
via























































