Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo akimsikiliza mkuu wa kikundi cha kukuna nazi ikiwa washiriki ni washindi katika makundi mbalimbali walioshindanishwa kukuna nazi. Mashindano hayo yanafanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika maonesho ya Tamasha la JAMAFEST.Ikiwa wamepata washindi wa tatu kutoka makundi tiofauti wakiwa wananwake wawili pamoja na mwananume mmoja.
Washiriki wa kukuna nazi wakisubiri filimbi ipigwe katika mashindano ya kukuna nazi wakiwa na kipimo cha ulaini wa nanzi pamoja na atakayewahi kumaliza na ikiwa safi. Washiriki ni washindi katika makundi mbalimbali walioshindanishwa kukuna nazi. Mashindano hayo yanafanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika maonesho ya Tamasha la JAMAFEST.
Washiriki wa mchezo wa kusuka ukiri wakicheza mchezo wao wa asili kusuka ukili. Hii ni katika Tamasha la JAMAFEST linaloendelea kufanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo akiangalia jinsi wasuka ukili walivyofanikiwa kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa kutumia ukili. Hii ni katikaTamasha la JAMAFEST linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika maonesho ya Tamasha la JAMAFEST.
Mambo ya Utamaduni yakioneshwa. Hapa ni Mishale na Mikuki.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo akiangalia meza na viti vilivyotengenezwa na Mianzi. Yote hayo ni katika tamasha la JAMAFEST linaloendelea kufanyika katika uwanja wa Taiafa jijini Dar es Salaam.
Utamaduni na sanaa ya Matanzania.
Mambo ya utamaduni kutoka Burundi.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2mKVWbW
via








