
Hatua hiyo inafanya Benki ya Exim Tanzania kuwa benki ya kwanza miongoni mwa benki za sekta binafsi hapa nchini zilizofanikiwa kuunganisha benki nyingine na hivyo kuifanya kuwa miongoni mwa benki tano kubwa hapa nchini ikiwa na ukwasi wa kiasi cha Tsh 1.7 Trilioni.
“Tunafurahishwa na ongezeko kubwa la wa wateja wa aina tofauti ambao watajiunga na familia ya benki ya Exim na tunawahakikishia kuwa tunafurahi kuwa nao kwenye safari yetu na tunajitoa kuhakikisha kwamba wanaendelea kufurahia huduma zenye ubunifu kutoka kwetu.”
”Wateja wakiwa ni sehemu muhimu zaidi ya biashara yetu, tunaahidi kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha wanafurahia huduma zetu,” Alisema Bwana Jaffari Matundu, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim.
Kwa mujibu wa Bw. Matundu hatua hiyo inakwenda sambamba na msimamo wa Rais Dk John Magufuli ambae amekuwa akisisitiza juu ya umuhimu wa kuwa na benki kubwa zaidi na ndogo nchini kwa kuwa ni hatua muhimu kwa afya ya kifedha katika ukuaji wa uchumi hususani katika kutoa huduma kamili na zenye ubunifu kwa wateja.
“Tanzania ina benki nyingi ukilinganisha na mataifa mengine ikiwemo Afrika Kusini na Nigeria. Sekta ya benki imekuwa ikishuhudia uunganishwaji wa mabenki ambao mwisho wa siku utaziacha benki zikiwa na uwezo wa kusukuma ukuaji wa uchumi kikamilifu. ”
“Dar es salaam ni soko muhimu kwa Benki ya Exim na hivyo uwepo wa tawi jipya la Mkwepu ambalo lenye teknolojia, ubunifu na muundo ambao utawawezesha wateja kukutana na maafisa wa benki kwa njia ambayo inawafaa na katika mazingira ambayo ni yanafikika kwa wote,” alisema.
Aidha Bw Matundu alisema mchanganyiko wa benki binafsi na zile za umma zilizosambaa kote nchini utahakikisha kuwa kuna mtiririko mzuri wa huduma za kifedha.
“Wajasiriamali watakuwa wamehakikishiwa upatikanaji wa kutosha wa mitaji inayohitajika kupanua biashara zao, ambayo itasababisha kasi kubwa ya ongezeko la ajira na hivyo kupunguza kabisa tatizo la ukosefu wa ajira nchini,” alisema
Ujio wa tawi hilo jipya unaifanya benki ya Exim Tanzania kuwa kuwa na jumla ya matawi 33 kote nchini.
Kwa zaidi ya miaka 22, benki ya Exim imefanikiwa kupata hadhi ya kuwa benki kimbilio si tu Tanzania bali pia nje ya nchi ambapo imeweza kujitanua kwa kuanzisha matawi yake ikiwemo nchi za Djibouti, Comoros na Uganda.

from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2qr4BSV
via






