WEMA SEPETU ADAIWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA

Admin Updates11 years ago14 Views




Skendo ya mastaa mbalimbali Bongo kutajwa katika biashara na
usafirishaji wa madawa ya kulevya ‘unga’ linazidi kuchukua sura mpya
ambapo tayari majina ya wasanii wawili wakubwa, Wema Isaac Sepetu na
Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ yametajwa huku kinachowaponza
kikijulikana.




Habari zinadai kuwa mastaa hao wameanza kujutia tambo zao za kutangaza
utajiri walionao hivyo kuibua maswali kuwa huenda wana uhusiano na
wafanyabiashara wa dawa za kulevya ikiaminika ndiyo njia ya haraka ya
utajiri.


WEMA
Inadaiwa kuwa kitendo cha Wema kutangaza kununua
nyumba, magari ya kifahari na kutapanya fedha ndiko kulikomponza na
sasa anatajwa na wengi vinywani mwao juu ya kuhusika katika biashara
hiyo haramu.




Kuna madai kuwa bosi huyo wa Endless Fame Productions
amehojiwa juu ya suala hilo lakini meneja wake, Martin Kadinda
alikanusha uvumi huo.




DIAMOND

Wiki iliyopita, Diamond aligeuka gumzo baada ya kuripotiwa
akihusishwa na biashara hiyo huku ikidaiwa kuwa kinachomponza ni utajiri
alioupata ghafla.




Ilidaiwa kuwa kitendo cha kutangaza kununua nyumba
takriban tano jijini Dar, kumiliki kiasi cha Sh. bilioni moja kwenye
akaunti na kuendesha magari ya kifahari ndivyo vilivyochangia watu
kugeuzia antena za runinga zao kwake kutaka kujua ni matunda ya muziki
tu au kuna kingine.




Madai ya jina la Diamond kutajwa katika saga hilo
yalikwenda mbele zaidi ikielezwa kuwa kitendo cha kusafiri mara nyingi
nje ya nchi huku akipiga picha na watu wanaosemekana kujihusisha na
biashara hiyo nacho kilimponza.




Kwa upande wake, Diamond alisema kuwa
hakuna mtu asiyejua namna anavyotafuta fedha kwa jasho juani hivyo watu
wakimuona akila kivulini lazima wakumbuke kuwa amechumia juani na hajui
chochote juu ya dawa hizo.

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...